Pata taarifa kuu

Liberia: Waangalizi wa kimataifa watoa pongezi kwa kufanyika uchaguzi wa amani

Nairobi – Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa nchini Liberia, wameipongeza nchi hiyo kwa kufanya uchaguzi wa amani wa duru ya pili, wakati huu wagombea wawili rais George Weah na mpinzani wake Joseph Boakai, wakikaribiana kwa kura.

Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kwanza tangu Umoja wa Mataifa ulipohitimisha ujumbe wa kulinda amani nchini Liberia
Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kwanza tangu Umoja wa Mataifa ulipohitimisha ujumbe wa kulinda amani nchini Liberia REUTERS - CARIELLE DOE
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya awali yanaonesha kiongozi wa upinzani Joseph Boakai anaongoza kwa asilimia 50.58 dhidi ya Rais George Weah ambaye ana asilimia 49.42.

Katika duru ya kwanza, wagombea hao walishindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, hii ikiwa ni kama marudio ya uchaguzi wa mwaka 2017 ambapo baada ya duru ya pili, Weah aliibuka mshindi kwa zaidi ya asilimia 61 ya kura.

Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kwanza tangu Umoja wa Mataifa ulipohitimisha ujumbe wa kulinda amani nchini Liberia.

Ujumbe huo uliundwa baada ya zaidi ya watu 250,000 kufariki katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1989 na 2003.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.