Pata taarifa kuu

Liberia: Kura za urais zinaendelea kuhesabaiwa

Nairob – Kura zimeendelea kuhesabiwa nchini Liberia, siku moja baada ya uchaguzi wa duru ya pili kati ya rais George Weah na mpinzani wake Joseph Boakai, ambaye kwa mujibu wa matokeo ya awali anaongoza kwa kura chache.

Wakati huu kura zikiwa zimehesabiwa kutoka katika vituo elfu 1 na 315 kati ya 5,890 Boakai alikuwa mbele kwa asilimia 50.7 ya kura
Wakati huu kura zikiwa zimehesabiwa kutoka katika vituo elfu 1 na 315 kati ya 5,890 Boakai alikuwa mbele kwa asilimia 50.7 ya kura AFP - AHMAD GHARABLI,SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo la upigaji kura lilikamilika bila ya kuripotiwa matukio yoyote vya ghasia ambapo wapiga kura zaidi ya milioni 2.4 walishiriki.

Waangalizi wa uchaguzi huo wanatarajia matokeo kuwa ya ushindani hasa baada ya duru ya kwanza, wagombea hao kupata asilimia 43 ya kura zote.

Wakati huu kura zikiwa zimehesabiwa kutoka katika vituo elfu 1 na 315 kati ya 5,890 Boakai alikuwa mbele kwa asilimia 50.7 ya kura, kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Davidetta Browne Lansanah.

Kulingana na sheria za Liberia, tume ya uchaguzi inazo siku 15 tangu kumalizika kwa zoezi ya kupiga kura, kumtangaza mshindi, ingawa anaweza kutangazwa mapema zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.