Pata taarifa kuu

Somalia kupokea mkopo wa dola bilioni 1 kutoka IMF

Nairobi – Nchi ya Somali, inatarajia kupokea mkopo zaidi kutoka kwa shirika la fedha duniani IMF, wakati huu bajeti yake ikikadiriwa kufikia dola bilioni 1.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa makadirio ya bajeti yake kufikia dola za Marekani bilioni 1
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa makadirio ya bajeti yake kufikia dola za Marekani bilioni 1 AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa makadirio ya bajeti yake kufikia dola za Marekani bilioni 1.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya fedha yaliyoidhinishwa wiki iliyopita na baraza la mawaziri, bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka ujao, itafikia dola bilioni 1, ikizidi bajeti ya mwaka uliopita.

Waziri wa fedha wa Somalia, Bihi Iman Egal, amesema anatarajia bajeti ya mwaka 2024 mapato yake yatokane na kodi za ndani pamoja na misaada ya kimataifa.

Nchi ya Somalia ni miongoni mwa mataifa mengine 7 ya Afrika yanayotarajiwa kupewa mkopo na IMF, ikiwemo, DRC, Rwanda, Tanzania, Gambia, Comoro na Senegal

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.