Pata taarifa kuu

Nchi ambazo ni makazi ya misitu mikuu mitatu ya mvua duniani kushirikiana kumaliza ukataji miti

Nchi ambazo ni makazi ya misitu mikuu mitatu ya mvua duniani mwishoni mwa wiki iliyopita, zimekubaliana kushirikiana ili kumaliza ukataji miti na kulinda bayoanuwai lakini zikashindwa kufikia makubaliano dhabiti ya kulinda udhibiti wa kaboni.

Ukataji miti uliongezeka kwa 4% ulimwenguni kote mnamo 2022
Ukataji miti uliongezeka kwa 4% ulimwenguni kote mnamo 2022 AFP PHOTO DESIREY MINKOH
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano haya yalifikiwa katika siku siku ya mwisho ya mkutano wa kilele wa Mabonde Matatu ulioandaliwa na Congo Brazaville, mkutano uliowaleta pamoja marais, Mashirika yasiyo ya kiserikali, wataalam wa kiufundi, na maafisa wa sekta ya fedha ili kuimarisha utawala na uhifadhi wa Amazon, bonde la Kongo, na misitu ya Kusini Mashariki mwa Asia.

Aidha nchi hiyo zilitambua umuhimu wa ushirikiano na kukubaliana kuendeleza njia za kulinda misitu katika mpango wenye vipengele saba.

Wataalamu wanasema mabonde hayo ni makazi ya theluthi mbili ya viumbe hai duniani, lakini uharibifu unaofanyika umesababisha kuongezeka kwa hewa kaa inayoongeza joto na kuathiri hatua za kufikia malengo ya hali ya hewa duniani.

Ukataji miti uliongezeka kwa 4% ulimwenguni kote mnamo 2022, kulingana na ripoti ya Oktoba inayoonyesha nchi zilikwenda mbali zaidi kutoka kwa ahadi zilizotolewa mwaka 2021 na Umoja wa Mataifa wa kusitisha na kudhibiti hasara na uharibifu ifikapo 2030

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.