Pata taarifa kuu

Vita nchini Sudan: Mazungumzo kuanza tena chini ya upatanishi wa Marekani na Saudia

Mazungumzo yanatarajiwa kurejelewa Alhamisi hii huko Jeddah, nchini Saudi Arabia, kati ya wajumbe kutoka jeshi la Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na kiongozi wa wanamgambo, Jenerali Mohamad Hamdane Daglo, anayejulikana kwa jina la "Hemedti". Hadi sasa, majaribio mbalimbali ya upatanishi yameshindwa, na kuwezesha tu mapatano mafupi tu ya kusitisha mapigano kufikiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Faisal bin Farhan (katikati) akihudhuria kutiwa saini kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya wawakilishi wa jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka, tarehe 21 Mei 2023 huko Jeddah.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Faisal bin Farhan (katikati) akihudhuria kutiwa saini kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya wawakilishi wa jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka, tarehe 21 Mei 2023 huko Jeddah. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Ni kurejelewa kwa mazungumzo kati ya jeshi na wanamgambo ambayo yatafanyika chini ya uangalizi wa Marekani na Saudi Arabia. "Tunakubali mwaliko wa Jeddah," jeshi lilisema katika taarifa siku chache zilizopita, na kuongeza kuwa kuanza tena kwa mazungumzo hakumaanishi kusitishwa kwa vita. Kwa upande wao, wanajeshi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka waliitikia vyema wito huo siku ya Jumatano, wakibaini kwamba wanataka kuwaondolea mateso raia wa Sudan na wanataka kuwezesha kuwasili kwa misaada ya kibinadamu kwa raia.

Viongozi wa pande hizo mbili hawatakuwepo. "Kwa hivyo ni vigumu kutumaini mafanikio yoyote ya kidiplomasia," anaelezea Magdi El Gizouli, mtafiti katika Taasisi ya Rift Valley. "Pande hizo zinapaswa kuzingatia uwezekano wa kusitisha mapigano na uanzishwaji wa eneo la usalama kwa aminajili ya kupitisha misaada. " Hayo yalitangazwa Jumapili na Luteni Jenerali Shams Eddin Kabachi, naibu kamanda wa vikosi vya jeshi la Sudan, wakati wa ukaguzi wa wanajeshi huko Port Sudan. Utafutaji wa suluhu la kisiasa utatokea tu katika "awamu ya mwisho" ya mazungumzo.

Kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani ikiitwa Twitter). jeshi la Sudan limeongeza kwamba "mazungumzo hayamaanishi usitishwaji mapigano na leno kuu la raia wa Sudan ni kuwaangamiza waasi. " Kwa upande wa RSF, hakuna maoni yoyote ambayo yametolewa kwa sasa, lakini mapigano huko Khartoum yameongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni. Kila upande ukijaribu kupata misimamo yake kabla ya mazungumzo yoyote kuanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.