Pata taarifa kuu
HAKI-HIFADHI

CNDA: Vita Darfur Kusini vinahalalisha utoaji wa hifadhi ya ukimbizi nchini Ufaransa

Siku ya Jumatatu, Mahakama ya Kitaifa ya Ukimbizi (CNDA), mahakama maalumu ya utawala ya Ufaransa, ilitangaza kwamba itawaruhusu raia wa Darfur Kusini, eneo lililoathiriwa vibaya na vita, kunufaika na haki ya hifadhi ya ukimbizi.

Nyala ni mji mkuu wa Darfur Kusini, eneo la Sudan linalopakana na Sudan Kusini. Nchi hizo mbili zimefungua tena mpaka wao mnamo Oktoba 1, 2021.
Nyala ni mji mkuu wa Darfur Kusini, eneo la Sudan linalopakana na Sudan Kusini. Nchi hizo mbili zimefungua tena mpaka wao mnamo Oktoba 1, 2021. Β© Wikimedia Commons CC BY-SA 4.0 Taha hussain33
Matangazo ya kibiashara

Ni kwa kutoa uamuzi unaofaa kwa "manufaa ya ulinzi tanzu unaotolewa na sheria za Ulaya" kwa Msudan kutoka eneo la Khireyga ndipo CNDA ilifikiria kutathmini hali ilivyo kwa Wasudan walio katika mazingira kama hayo. Na kama aina hii ya uamuzi wa CNDA, ambayo inakata rufaa juu ya maombi ya hifadhi ya ukimbizi, inaweka mfano kwa kesi zote zinazofanana, raia wa Sudan Kusini wanaweza kupata hifadhi nchini Ufaransa.

Mwombaji aliomba hifadhi ya ukimbizi na akielezea kuwa na hofu dhidi ya mamlaka ya nchi yake kutokana na kuwa ni kutoka kabila la Dadjo na maoni ya kisiasa yanayodaiwa kuhusishwa naye. Vielelezo visivyotosheleza kwa mahakama ambayo hata hivyo ilitoa hifadhi ya ukimbizi kwa sababu ya eneo ambalo mtu huyo anatoka.

Houda Ibrahim

Ili kuhalalisha uamuzi wake, mahakama ilitangaza kwamba nchini Sudan, eneo la Darfur Kusini linakabiliwa na "hali ya ghasia zisizokoma" hali ambayo ilifanya ifungue njia kwa ajili ya ulinzi wa raia wake chini ya hifadhi ya ukimbizi nchini Ufaransa, inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Mahakama ya Kitaifa ya Hifadhi ya ukimbizi. Mahakama ilizingatia kwamba mtu huyu alikuwa na hatari kubwa ya tishio kubwa kwa mtu au maisha yake ikiwa atarudi katika jimbo lake la asili, kama raia.

Tangu Aprili 15, tarehe ambayo vita vilizuka kati ya wanajeshi wa Sudan na wanamgambo, mikoa kadhaa ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na Darfur Kusini imekumbwa na hali ya ghasia kali zisizokoma. Zaidi ya hayo, ghasia za kikabila zimetokea leo huko Darfur Kusini, kati ya makabila mawili yenye silaha kutoka kwa vikosi vya msaada wa haraka, RSF. Kulingana na vyanzo vya ndani, mapigano hayo yamesababisha makumi ya watu kuuawa na wengine kujeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.