Pata taarifa kuu

Nigeria: Mahakama kuamua kesi ya uchaguzi wa urais kesho

Mahakama ya Juu nchini Nigeria, kesho itaamua kesi ya wanasiasa wa upinzani, wanaopinga ushindi wa rais Bola Tinubu, kufuatia uchaguzi wa urais mwezi Februari.

Mahakama ya Juu nchini Nigeria
Mahakama ya Juu nchini Nigeria © guardian
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya Mahakama jijini Abuja, imethibitisha hatua hiyo, uamuzi ambao unatarajiwa kuwa wa mwisho kuhusu mzozo wa mshindi wa uchaguzi huo.

Waliokuwa wagombea, Atiku Abubakar kutoka chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic Party na Peter Obi wa chama cha Leba, walikataa rufaa kwenye Mahakama hiyo ya juu mwezi Septemba, baada ya Mahakama ya chini kuamua kuwa rais Tinubu alishinda uchaguzi huo kwa haki.

Wawili hao wanaitaka Mahakama hiyo kufuta ushindi wa Tinubu na kuangiza kufanyika kwa uchaguzi mpya, kwa madai kuwa uchaguzi wa Februari haukuwa huru na haki, licha ya matokeo hayo kukubaliwa na mataifa ya Magharibi.

Tangu kuanza kwa mfumo wa kidemokrrasia nchini Nigeria, baada ya kumalizika kwa uongozi wa kijeshi mwaka 1999, matokeo ya uchaguzi wa urais yamekuwa yakipingwa lakini Mahakama haijawahi kufuta ushindi wa aliyetangazwa mshindi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.