Pata taarifa kuu

DRC: Wahadhiri wa vyuo vikuu ambao hawajalipwa mishahara walalamika

Baadhi ya Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao wanadai mishahara yao wameelelezea hasira yao kufuatia miaka kadhaa kwa kutolipwa mishahara. Baadhi yao hawajalipwa kwa miaka kadhaa. Walifanya maandamano siku ya Ijumaa, Septemba 22, katika jengo la serikali kunakopatikana Wizara ya Bajeti.

Chuo Kikuu cha Kinshasa, DRC.
Chuo Kikuu cha Kinshasa, DRC. Wikimedia/Humprey J. L. Boyelo
Matangazo ya kibiashara

Walikuwa makumi ya wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kinshasa (UNIKIN), kikubwa zaidi nchini, kudai haki za mamia kadhaa nchini kote. Wanaahidi uhamasishaji mwingine ikiwa serikali haitajibu.

Akihojiwa na RFI, David Lubo, Mwenyekiti wa Chama cha wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kinshasa, anashtumu nia mbaya ya viongozi katika nchi ambapo bajeti nyingi hutumiwa na taasisi za kisiasa.

"Huzuni"

“Tatizo la wahadhiri wapya ambao hawajalipwa ni kubwa. Kinachohuzunisha na kutisha ni kwamba shida zinatukumba sote. Kuna hata wengine waliokufa katika mazingira kama haya. Inasikitisha kwamba tuko katika mji mkuu na kwamba tunafanya miaka miwili, mitatu, minne, mitano bila kulipwa. Sio siri. Profesa wa chuo kikuu nchini Kongo mshahara wake uko chini ya mfyagiaji katika wizara ya Bajeti na Fedha. Hili ndilo janga tunalokumbana nalo. Je, watawala wana matatizo hasa na walimu? Hata wale wanaolipwa, ni walimu wachache sana wanaolipwa kulingana na shahada zao.

“Aibu kuwa tajiri”

Uko mhadhii wa kawaida na bado unalipwa kama mhadhiri msaidizi. Tunasema kwamba ni nia mbaya. Bajeti inawahusu wale walio madarakani pekee. tabaka zingine zote zimeachwa nyuma, ikiwa ni pamoja na walimu. Ni lazima waone aibu kuwa matajiri mbele ya umati wa wapiga kura wao, walioshushwa hadhi, fukara, wanaonyonywa siku baada ya siku. Ikiwa mwaka 2024 hatutawapa walimu zaidi ya kile wanachopokea leo, tutakabiliwa na madhara makubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.