Mazungumzo kuhusu ujenzi wa bwawa la Ethiopia yamerejelewa
Ethiopia imesema imeanza awamu ya pili ya mazungumzo kati yake na mataifa ya Misri na Sudan kuhusu ujenzi wa bwawa lenye utata linalojengwa na Addis Ababa katika Mto Nile, chanzo cha mzozo kati ya mataifa hayo matatu.
Imechapishwa:
Kupitia katika ukurasa wa X, zamani ukijulikana kama twitter, wazira ya mambo ya kigeni ya Ethiopia imethibitisha kurejelewa kwa mazungumzo hayo.
Mwezi huu Ethiopia ilitangaza kukamilisha kujaza maji katika bwawa la Grand Renaissance, hali ambayo ilikashifiwa vikali na Cairo ambayo ilisema hatua hiyo ilikuwa kinuyme cha sheria.
Misri na Sudan zimeibua wasiwasi kuwa mradi huo mkubwa mwenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 4.2, utapunguza viwango vya maji zinazopokea kutoka mto Nile.
Mtaifa hayo mawili yamekuwa yakitaka Addis Ababa kusitisha mradi huo hadi pale ambapo makubaliano yataafikiwa kati ya wahusika wakuu kwenye mzozo huo.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed walikubaliana mwezi Julai kutafuta suluhu katika kipindi cha miezi minne kabla ya kurejelewa kwa mazungumzo mwezi Agosti.