Pata taarifa kuu

Rais wa Senegal anaona suluhisho la kidiplomasia 'bado linawezekana' nchini Niger

Rais wa Senegal Macky Sall amesema Alhamisi kwamba "bado inawezekana" kuelekea kwenye suluhu la kidiplomasia nchini Niger karibu miezi miwili baada ya mapinduzi yaliyofanywa na jeshi lililompindua rais Mohamed Bazoum.

Rais wa Senegal Macky Sall akihojiwa mjini New York mnamo Septemba 21, 2023.
Rais wa Senegal Macky Sall akihojiwa mjini New York mnamo Septemba 21, 2023. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ambayo Senegal ni sehemu yake, imekuwa ikitishia viongozi wa mapinduzi kuingilia kijeshi tangu Julai 30 ili kumrejesha Rais Bazoum katika majukumu yake.

Alitangaza kuwa siku na taratibu za operesheni hiyo ziliamuliwa, hata hivyo akiipa kipaumbele njia ya kidiplomasia.

"Nina matumaini kwamba sababu hatimaye itashinda (...), kwamba bado inawezekana kuelekea kwenye suluhu," amesema rais Sall katika mahojiano na vyombo vya habari vya Ufaransa RFI na France 24. Amewasihi wanajeshi walio madarakani " msitufanye (sisi) kuchukuwa uamuzi wa mwisho ambao utakuwa uingiliaji wa kijeshi".

"Chaguo hili la mwisho la kijeshi linaweza tu kufanywa wakati, kwa kweli, njia zote zitakuwa zimeshindwa," amesema katika mahojiano haya yaliyotolewa kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York.

Ninajua kwamba Nigeria, ambayo Rais wake Bola Tinubu ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), "inafanya kila kitu kutafuta suluhu kupitia njia za kidiplomasia", amesema.

"Nasubiri atufahamishe matokeo ya mbinu zake mbalimbali ili hatimaye tutathmini na kupitisha uamuzi wa pamoja," ameongeza. Akimzungumzia Bw. Bazoum, amehakikisha kwamba hatungeweza kuruhusu "rais aliyechaguliwa achukuliwe mfungwa nyumbani kwake."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.