Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Bunge laidhinisha kutumwa kwa jeshi nchini Niger

Nairobi – Bunge la mpito nchini Burkina Faso, limeidhinisha azimio la kutumwa kwa jeshi nchini Niger, inayokabiliwa na uwezekano wa kushambuliwa na kikosi cha Jumuiya ya ECOWAS iwapo, haitarejesha uongozi kwa rais Mohammed Bazoum.

Hatua hii ya wabunge inakuja, baada ya Jumamosi iliyopita wakuu wa nchi za Niger, Burkina Faso na Mali kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kijeshi
Hatua hii ya wabunge inakuja, baada ya Jumamosi iliyopita wakuu wa nchi za Niger, Burkina Faso na Mali kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kijeshi AFP - ALEXEY DANICHEV
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa azimio hilo, Burkina Faso ambayo pia inaongozwa na wanajeshi, inaweza kutuma kikosi chake kwa kipindi cha miezi mitatu, ambacho kinaweza kuongezwa.

Wabunge wameazimia kuwa, jeshi lake litakwenda nchini Niger, iwapo nchi hiyo itashambuliwa, kwa lengo la kuisaidia jirani yake.

Hatua hii ya wabunge inakuja, baada ya Jumamosi iliyopita wakuu wa nchi za Niger, Burkina Faso na Mali kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kijeshi.

Tarehe 26 mwezi Julai, jeshi nchini Niger, lilimpindua rais Bazoum kwa madai ya kushindwa kuimarisha usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Jumuiya ya ECOWAS imetishia kutuma jeshi lake, kuhakikisha kuwa rais Bazoum anarejeshwa madarakani, iwapo uongozi wa kijeshi hautarejesha madaraka kwa uongozi wa kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.