Pata taarifa kuu

Waziri Mkuu wa Gabon ahutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Waziri Mkuu wa Gabon, Raymond Ndong Sima, aliyeteuliwa na jeshi lililochukua mamlaka mwishoni mwa mwezi Agosti, aamelihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano.

Raymond Ndong Sima, Waziri Mkuu wa Gabon.
Raymond Ndong Sima, Waziri Mkuu wa Gabon. Photo : Anthony Lattier/RFI
Matangazo ya kibiashara

Gabon ni miongoni mwa wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa kipindi cha miaka miwili hadi mwisho wa mwaka 2023.

Swali la ujio wake kwenye Umoja wa Mataifa ambapo Mkutano Mkuu wa Mwaka unafanyika wiki hii, lilikuwa likisubiriwa wakati Agosti 30, jeshi la Gabon lilimpindua rais Ali Bongo Ondimba, madarakani kwa miaka 14.

Mapinduzi haya yalishutumiwa na jumuiya ya kimataifa.

Katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Raymond Ndong Sima amehimiza kukomeshwa kwa vita nchini Ukraine, akisisitiza athari za mzozo huu ambao unazidisha "adhabu ya kibinadamu duniani kuhusu njaa, hatari, dhiki, hofu".

"Sauti mbadala ya vita inawezekana, ni lazima ipatikane kupitia njia zilizopo pamoja na maazimio husika ya baraza hili," amesema pia.

Alikariri wito wa nchi yake "kwa pande zote kwa mazungumzo kwa nia njema kumaliza vita hivi."

"Kila kitu lazima kifanyike ili kupunguza na kuunda mazingira kwa minajili ya  kutumwa diplomasia," amesema Raymond Ndong Sima, kiongozi wa upinzani wa zamani nchini Gabon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.