Pata taarifa kuu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, atangaza kujiuzulu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, raia wa Ujerumani, ametangaza Jumatano kwamba amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ameonya juu ya hatari ya "vita vya wenyewe kwa wenyewe" katika nchi hii iliyoharibiwa na migogoro ya vita.

Volker Perthes alikuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan kwa miaka miwili na nusu na aliongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa, UNAMIT, ulioundwa mwezi Juni 2020 ili kuunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia nchini Sudan baada ya kuanguka kwa utawala wa Omar al-Bashir mwaka mmoja uliotangulia.
Volker Perthes alikuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan kwa miaka miwili na nusu na aliongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa, UNAMIT, ulioundwa mwezi Juni 2020 ili kuunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia nchini Sudan baada ya kuanguka kwa utawala wa Omar al-Bashir mwaka mmoja uliotangulia. REUTERS - EL TAYEB SIDDIG
Matangazo ya kibiashara

"Namshukuru Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nafasi hii na kwa imani aliyoniweka kwangu, lakini nimemwomba anipunguzie kazi hii," Bw. Perthes amesema baada ya kutoa ripoti yenye huzuni kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akishtumu pande hasimu zinazokinzana nchini humo, jeshi la Sudan na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF).

"Kilichoanza kama mzozo kati ya makundi mawili ya kijeshi kinaweza kugeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo kamili," amesema, akisisitiza kwamba "mapigano hayaonyeshi dalili za utulivu na hakuna upande unaoonekana kuwa karibu" na ushindi.

Watu 40 wauawa Nyala

Takriban watu 40 wameuawa siku ya Jumatano huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini, katika mashambulizi ya anga ya jeshi, chanzo cha hospitali na mashahidi wameliambia shirika la habari la AFP.

Bw. Perthes alikuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan kwa miaka miwili na nusu na aliongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa, UNAMIT, ulioundwa mwezi Juni 2020 ili kuunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia nchini Sudan baada ya kuanguka kwa utawala wa Omar al-Bashir mwaka mmoja uliotangulia.

Alioneka adui kwa kiongozi mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, ambaye alitoa wito wa kufutwa kazi, akimlaumu kwa vita vilivyozuka katikati ya mwezi Aprili na wanamgambo wa Jenerali Mohamed Hamdane Daglo.

"Tunapaswa kufahamisha pande zinazohasimiana waelewe kwamba hawawezi kuchukua hatua bila kuadhibiwa na kwamba watalazimika kujibu kwa uhalifu uliofanywa," amesema Bw. Perthes.

Kulingana na takwimu alizozitaja, takriban watu 5,000 wameuawa tangu kuanza kwa mzozo huo Aprili 15 na zaidi ya 12,000 kujeruhiwa, takwimu ambazo ni chini ya uhalisia kulingana na Bw. Perthes.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.