Pata taarifa kuu

Misri yakasirishwa na tamko la Ethiopia kujaza bwawa kutumia maji ya Mto Nile

Misri imekarishwa na tangazo la Ethiopia, kuwa limefanikiwa kujaza bwawa lake kubwa la Grand Ethiopian Renaissance, kwa ajili ya mradi wa kuzalisha umeme.

Bwawa kubwa la Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015.
Bwawa kubwa la Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka 2011, Ethiopia imekuwa kwenye mzozo na Misri, lakini pia Sudan kuhusu mradi wake mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji ya mto Nile.

Mradi huo umbali wa Kilomita 30 kutoka Sudan, unatarajiwa kuzalisha umeme wa Megawati 6,000.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kupitia ukurasa wake wa X, ametangaza kujazwa kwa êneo la nne la bwawa hilo la umeme, kitendo ambacho amesema  kimefanyika kwa mafanikio makubwa.

Hata hivyo, Misri inasema mradi huo wa Ethiopia, utaathiri upatikanaji wa maji kutoka mto huo.

Wizara ya Mambo ya nje, jijini Cairo imesema hatua ya Ethiopia ni dharau kwa maslahi ya nchi zingine,zinazotegemea maji ya mto Nile.

Hata hivyo, Ethiopia imekuwa ikijitetea na kuendelea na mradi wake wenye thamani ya Dola Bilioni 4.2 kwa kile inachosema, hautaathiri mgao wa maji unaokwenda nchini Misri.

Mazungumzo kati ya Ethiopia, Sudan na Misiri kutatua mvutano huo, yamekuwa yakifanyika bila mafanikio yoyote. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.