Pata taarifa kuu

Burhan azuru Qatar kutafuta uungwaji mkono wakati vita vikiendelea

Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan amekutana na kufanya mazungumzo na Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani,, ikiwa ni ziara yake ya tatu nje ya nchi baada ya kuzuka kwa vita nchini mwake mwezi Aprili.

Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan akiwasili jijini Doha, 07/09/2023.
Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan akiwasili jijini Doha, 07/09/2023. REUTERS - JOK SOLOMUN
Matangazo ya kibiashara

Akiwa  jijini Doha, al-Burhan amejadiliana na Emir Al Thani, na kumwelezea hali inavyoendelea katika nchi yake, wakati huu jeshi likipambana na wanamgambo wa RSF.

Kabla ya kwenda nchini Qatar, kiongozi huyo wa kijeshi alikuwa katika nchi jirani ya Sudan Kusini lakini pia alikwenda jijini Cairo nchini Misri, kushauriana na rais Abdel Fattah El-Sisi.

Wachambuzi wa masuala ya Sudan wanasema  lengo la ziara ya Jenerali al-Burhan ni kuomba uugwaji mkono dhidi ya kundi la RSF.

Kabla ya ziara hiyo, Burhan alitangaza kukivuja kikosi cha RSF anachosema kimeisaliti nchi baada ya kuanza vita. Kikosi cha RSF kinaoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo, ambaye alikuwa msaidizi wa Burhan kwenye serikali ya kijeshi.

Vita nchini Sudan kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa na Umoja wa Mataifa, vimesabbaisha vifo vya zaidi ya watu Elfu tano na maelfu kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.