Pata taarifa kuu

Ethiopia: Watu 183 wameuawa katika mapigano jimboni Amhara

Nairobi – Karibia watu 183 wameuawa tangu mwezi Julai katika machafuko kwenye jimbo la Amhara nchini Ethiopia, umoja wa mataifa umethibitisha.

Karibia watu 183 wameuawa tangu mwezi Julai katika machafuko kwenye jimbo la Amhara nchini Ethiopia
Karibia watu 183 wameuawa tangu mwezi Julai katika machafuko kwenye jimbo la Amhara nchini Ethiopia © REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake UN imetoa wito kwa kusitishwa kwa mauaji na ghasia na ukiukaji wa haki za binadamu.

Hali ya wasiwasi iliaanza tena kushuhudiwa kaskazini mwa taifa hilo baada ya kusitishwa kwa mapigano mengine katika jimbo jirani la Tigray, mapigano yaliohusishwa pia wapiganaji kutoka katika jimbo la Amhara.

Mnamo Aprili serikali ya shirikisho ilitangaza kuwa imevunja vikosi vya mkoa kote nchini.
Mnamo Aprili serikali ya shirikisho ilitangaza kuwa imevunja vikosi vya mkoa kote nchini. AFP - EDUARDO SOTERAS

Msemaji wa ofisi ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa Marta Hurtado aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa wanasikitishwa sana na kuzorota kwa hali ya haki za binadamu katika baadhi ya mikoa ya Ethiopia.

UN imeeleza kuguswa zaidi na kinachoendelea katika eneo la Amhara, kufuatia kuongezeka kwa mapigano kati ya jeshi la Ethiopia na wanamgambo wa kikanda wa Fano hali iliyopelekea kutangazwa kwa hali ya dharura mnamo Agosti 4.

Watetezi wa haki wamebainisha aina mbalimbali za ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vya serikali katika eneo hilo
Watetezi wa haki wamebainisha aina mbalimbali za ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vya serikali katika eneo hilo © AFP - Eduardo Soteras

Mnamo Aprili serikali ya shirikisho ilitangaza kuwa imevunja vikosi vya mkoa kote nchini.

Hatua hiyo ilizua maandamano kutoka kwa wakaazi  wa Amhara ambao walisema itadhoofisha eneo lao.

Mapigano yalizuka mapema mwezi Julai kati ya jeshi la taifa na wapiganaji wa eneo hilo wanaojulikana kama Fano, na kusababisha mamlaka mjini Addis Ababa mnamo Agosti 4 kutangaza hali ya dharura ya miezi sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.