Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi DRC: Daktari Mukwege ahofia wizi wa kura na kutoa wito kwa Wakongo kuchukua hatua

Miezi minne kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu, Daktari Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel 2018 analaani ukiukaji wa taratibu za mchakato wa uchaguzi unaoendelea. 

Daktari Denis Mukwege.
Daktari Denis Mukwege. AFP - ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum katika Bukavu, William Basimike

Wakati wa hotuba kwa vijana wa mkoa wa Kivu Kusini siku ya Jumapili huko Bukavu, "Daktari huyu wa wanawake" hakutangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi ujao wa rais, kama walivyotarajia wengi, lakini alihisi kuwa muundo wa chaguzi za sasa unadhihirisha udanganyifu wa uchaguzi na kutoa wito kwa raia wa Kongo kutokubali haki yao ya msingi na matakwa yao kuangamizwa.

Mbele ya mamia ya vijana waliofika kumsikiliza katika Wakfu wa Panzi, Daktari Denis Mukwege alikashifu zaidi kadi za wapigakura ambazo tayari zilikuwa zimefutiliwa mbali muda tu baada ya kusahihishwa kwa sajili ya uchaguzi. Kwa mujibu wa Daktari Mukwege, hii ni ishara mbaya:

"Tunapokuwa na makosa ya aina hii, na kushindwa kukemea na kusema kwamba njia inayotuwezesha kufanya uchaguzi wetu tayari ina upendeleo, tunaweza kutarajia nini? Nadhani hasira kubwa leo ingekuwa kwa kila aliyefutiwa kadi za wapiga kura kujitokeza na kusema, "kama ulilipia kadi zisizo sahihi za wapiga kura, lazima uwajibike." Lakini tukinyamaza tukaenda kwenye chaguzi ambazo ziliandaliwa kwa kutapeliwa lazima nikuambie: soma historia ya Kongo utaona tangu mwaka 1885 hadi leo wakongo hawajawahi kuchagua viongozi wao. "

Daktari Mukwege ametoa wito kwa kuvunja ukimya wa kizalendo kwa ajili ya kuanzishwa upya kwa DRC. Anabaini kwamba ukimya wa Wakongo mbele ya maovu yao ni usaliti.

Hata hivyo, vijana waliokuwepo walihisi kuwa Denis Mukwege anashikilia mashaka hayo badala ya kuwa wazi kisiasa. Marie Sifa anaondoka kwenye chumba cha mkutano, alitarajia tangazo kubwa: "Ningependa azungumze kwa sababu kwa matendo yake, maneno yake, tunaona kwamba anastahili kuwa rais wa Jamhuri. Natamani angeweza kuwa muwazi, ingeweza kuwa bora zaidi. »

Wasaidizi wa Daktari Mukwege bado wanasema wanaamini kuwa Daktari Mukwege bado ana nia ya kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.