Pata taarifa kuu

Raia wa Zimbabwe wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais

Wakati huu wananchi wa Zimbabwe, wanaposubiri matokeo ya uchaguzi wa urais, uliofanyika siku ya Jumatano na kuendelea mpaka jana, polisi wanasema wamewakamata waangalizi 41 wa ndani.

Marekani imelaani kukamatwa kwa waangalizi hao
Marekani imelaani kukamatwa kwa waangalizi hao © Tsvangirayi Mukwazhi / AP
Matangazo ya kibiashara

Waangalizi hao kutoka vuguvugu la kupigania demokrasia, walikamatwa Jumatano usiku jijini Harare na vifaa vyao vya kazi kama tarakilishi na simu kuchukuliwa.

Polisi wanasema, wamechukua hatua hiyo kwa madai kuwa waangalizi hao walikuwa wanajumuisha matokeo ya urais, kitendo ambacho wanasema ni kinyume cha sheria.

Marekani imelaani kukamatwa kwa waangalizi hao, kitendo ambacho wizara ya mambo ya nje kupitia msemaji wake, Matthew Miller amesema ni kitendo cha kuzuia uchaguzi huru na haki.

Hatua hii imekuja, wakati huu upinzani ukidai mbinu chafu za kuiba kura, baada ya upigaji kura kucheleweshwa katika ngome zao, kwa lengo la kuwakatisha tamaa wapiga kura.

Tume ya uchaguzi ina hadi siku tano, kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais ambao ushindani mkubwa ni kati ya rais Emmerson Mnangangwa na Nelson Chamisa kutoka chama kikuu cha upinzani CCC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.