Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-HAKI

Ethiopia na Saudi Arabia kufanya uchunguzi wa pamoja kuhusu madai ya mauaji ya wahamiaji

Serikali ya Ethiopia imetangaza Jumanne kwamba itafanya uchunguzi wa pamoja na Saudi Arabia, kufuatia kuchapishwa kwa ripoti ya Human Rights Watch inayowashutumu walinzi wa mpaka wa Saudia kwa kuua "mamia" ya wahamiaji wa Ethiopia kati ya mwezi Machi 2022 na Juni 2023.

Wahamiaji wa Ethiopia wakishuka boti kwenye ufuo wa Ras al-Ara, Lahj, Yemen, wakiwa wamedhamiria kuingia nchini Saudi Arabia, Julai 26, 2019.
Wahamiaji wa Ethiopia wakishuka boti kwenye ufuo wa Ras al-Ara, Lahj, Yemen, wakiwa wamedhamiria kuingia nchini Saudi Arabia, Julai 26, 2019. © AP
Matangazo ya kibiashara

"Serikali ya Ethiopia itachunguza tukio hilo mara moja kwa ushirikiano na mamlaka ya Saudia," Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imesema katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani ikiitwa Twitter).

"Katika hatua hii mbaya, inashauriwa kujizuia na kutotoa kauli zisizo za lazima hadi uchunguzi utakapokamilika", inaongeza wizara hiyo na kuhakikishia kuwa "nchi hizo mbili licha ya janga hili la bahati mbaya, zinafurahia uhusiano wa muda mrefu na wenye ubora. ".

Katika ripoti iliyotolewa Jumatatu, Human Rights Watch (HRW) inasema walinzi wa mpaka wa Saudi Arabia waliwaua 'mamia' ya wahamiaji wa Ethiopia waliokuwa wakijaribu kuingia katika nchi hii  tajiri ya Ghuba kupitia mpaka na Yemen kati ya mwezi Machi 2022 na Juni 2023.

Mamlaka za Saudi arabia inapinga tukio hilo lililoripotiwa na HRW. Chanzo cha serikali kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba "ni madai yasio na msingi na si kutoka vyanzo vya kuaminika".

Umoja wa Ulaya, kupitia msemaji wa mkuu wa diplomasia Josep Borrell, ulionyesha "wasiwasi" wake kuhusu ripoti ya HRW.

"Tutazungumzia suala hili kwa mamlaka nchini Saudi Arabia na pia kwa mamlaka ya Houthi nchini Yemen," msemaji Peter Stano amesema. "Tunakaribisha tangazo la serikali ya Ethiopia la uchunguzi wa pamoja na mamlaka ya Saudi Arabia," ameongeza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Brussels.

Kulingana na ripoti ya shirika hilo lisilo la kiserikali, wahamiaji walishutumu vikosi vya Houthi kwa kushirikiana na walanguzi na kuwaibia pesa. Waasi hawa pia waliwahamishia kwenye kile ambacho wahamiaji wanakielezea kama vituo vya kizuizini.

Marekani, washirika wa muda mrefu wa utawala wa kifalme wa Ghuba, walitoa wito wa kufanyika uchunguzi siku ya Jumatatu.

Ripoti hii "inasumbua sana" na inatoa shutuma "zito sana," alisema msemaji wa Umoja wa Mataifa, akibainisha hata hivyo kwamba ni vigumu "kuthibitisha" madai haya.

Katika ripoti yake ya kurasa 73, HRW inategemea mahojiano na wahamiaji 38 wa Ethiopia waliojaribu kuingia Saudi Arabia kutoka Yemen, picha za satelaiti, video na picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii "au zilizokusanywa kutoka vyanzo vingine".

Waliohojiwa walizungumza kuhusu "silaha za vilipuzi" na ufyatuaji visa vya ufyatuliaji risasi, huku walinzi wa mpakani wa Saudi wakiwauliza Waethiopia "ni sehemu gani ya miili yao wangependelea kupigwa risasi".

Mamia ya maelfu ya Waethiopia wanafanya kazi nchini Saudi Arabia, wakati mwingine wakichukua "njia ya mashariki" kutoka Pembe ya Afrika hadi Ghuba, wakipitia Yemen, nchi maskini iliyo kwenye vita kwa zaidi ya miaka minane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.