Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: UN yatiwa wasiwasi kuhusu dhuluma za M23 na kuibuka kwa makundi ya kujilinda

Katika ripoti iliyotumwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwishoni mwa wiki hii Agosti 12-13 na ambayo ilivuja, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, hataji uwepo wa askari wa jeshi la Rwanda (RDF) pamoja na M23, waasi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, kwenye ardhi ya Kongo. Ripoti za hivi punde za wataalamu wa Umoja wa Mataifa hata hivyo zimepelekea nchi nyingi na Umoja wa Ulaya kulaani Rwanda kwa kuhusika kwake katika mzozo huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anasema ana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa makundi ya kujilinda nchini DRC kutokana na dhuluma za M23.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anasema ana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa makundi ya kujilinda nchini DRC kutokana na dhuluma za M23. AFP - ED JONES
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Katika ripoti yake ya kurasa 15, Antonio Guterres hajataja jeshi la Rwanda na uwepo kwenye ardhi ya DRC kwa kuilisaidia kundi la waasi la M23. Amejizuia kwa kukumbusha tu kwamba M23 "imeteka maeneo makubwa" ya mkoa wa Kivu Kaskazini. "Walianzisha mamlaka sawia na zisizo halali" katika maeneo mengi ya mkoa wa Kivu Kaskazini, ikiwa ni pamoja na kutoza ushuru na forodha.

Kulingana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, M23 'huwakamata watu kiholela' na kuwaua kikatili". Katika waraka huo, Antonio Guterres anaelezea wasiwasi wake: kuongezeka kwa makundi ya kujilinda yanayoundwa na raia wenye silaha wanaodai kupigana na M23. Hii inazua, kwake, "matatizo mengine ya usalama na inaweza kuchangia kwa mzunguko mpya wa vurugu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya kikabila na ulipizaji kisasi".

Picha anayotoa ya hali ya jumla iko wazi: mivutano ya kikanda imezidi kuwa mibaya katika mwaka mmoja, na "mamia ya maelfu ya raia wamelazimika kuyahama makazi yao" huko Kivu Kaskazini na Ituri. Na idadi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto "imeongezeka zaidi ya mara mbili kati ya mwaka 2021 na 2022".

Hata hivyo, Antonio Guterres ametangaza kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) umeingia "katika awamu yake ya mwisho" kabla ya kuondoka kwenye ardhi ya DRC, ambako wanajeshi wake wamekuwepo kwa miaka 25. Awamu madhubuti lakini ambayo haiendani na hali iliyopo, ambayo "inazorota kwa kasi" kulingana na mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambaye anataka "kuondoka kwa kasi kwa wanajeshi hao, lakini kwa kuwajibika". Kuondoka mapema "kutakuwa na madhara kwa raia ambao wanategemea misheni kuhakikisha ulinzi wao", amesisitiza.

Kuondoka kwa kundi la mwisho la wanajeshi wa MONUSCO kunaweza kufanyika, kwa mujibu wa Antonio Guterres, wakati mamlaka ya Kongo itakapochukua jukumu lao la msingi la ulinzi wa raia, na wakati idadi ya kutosha ya wanajeshi na polisi watatumwa kuhakikisha usalama wa raia walio hatarini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.