Pata taarifa kuu

Mapinduzi nchini Niger: Macron kuongoza baraza la ulinzi siku ya Jumamosi

Ufaransa ina wanajeshi 1,500 nchini Niger, inayochukuliwa kuwa mshirika mzuri wa Paris katika Sahel, na labda mojawapo ya washirika wa mwisho wa Paris katika Sahel.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alikuwa anatazamiwa kurejea kutoka Oceania usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, tayari amelaani "vikali" mapinduzi ya kijeshi yaliyompindua Mohamed Bazoum siku ya Jumatano.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alikuwa anatazamiwa kurejea kutoka Oceania usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, tayari amelaani "vikali" mapinduzi ya kijeshi yaliyompindua Mohamed Bazoum siku ya Jumatano. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron ataongoza kikao cha Baraza la Ulinzi na Usalama la Kitaifa kuhusu Niger saa tisa alaasiri leo Jumamosi, baada ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yalishuhudia mkuu wa kikosi cha walinzi wa rais kuchukua mamlaka, Ikulu ya Elysee ilitangaza siku ya Ijumaa.

Ufaransa, ambayo ilimaliza operesheni ya kupambana na ugaidi Barkhane na kujiondoa nchini Mali chini ya shinikizo kutoka kwa utawala wa kijeshi wa Bamako, kwa sasa ina wanajeshi 1,500 waliotumwa nchini Niger ambao wanafanya kazi na jeshi la Niger hadi sasa. Nchi hiyo, koloni la zamani la Ufaransa ambalo lilipata uhuru mwaka 1960, ni mojawapo ya washirika wa mwisho wa Paris katika Sahel.

Emmanuel Macron, ambaye alikuwa anatazamiwa kurejea kutoka Oceania usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, tayari amelaani "vikali" mapinduzi ya kijeshi yaliyompindua Mohamed Bazoum siku ya Jumatano.

Mapinduzi yaliyofanyika kinyume cha sheria

"Mapinduzi haya ni haramu kabisa na ni hatari sana kwa Waniger, kwa taifa la Niger, na kwa kanda nzima," Macron alisema. "Ndiyo maana tunatoa wito wa kuachiliwa kwa rais Bazoum na kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba," alisema kutoka Papua New Guinea.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa kwa upande wake ilithibitisha kwamba Ufaransa "haitambui mamlaka ya kijeshi" kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani.

Jenerali Tchiani alijihidhirisha kwenye televisheni ya umma siku ya Ijumaa kama "rais wa Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa taifa", baada ya mapinduzi ambayo alihalalisha kutokana na "kuzorota kwa hali ya usalama" nchini.

Baada ya Mali na Burkina Faso, Niger inakuwa nchi ya tatu katika ukanda wa Sahel, iliyokumbwa na mashambulizi kutoka kwa makundi yenye uhusiano na Islamic State na Al-Qaeda, kukumbwa na mapinduzi tangu 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.