Pata taarifa kuu

Mkutano wa Afrika na Urusi kuaanza leo mjini St. Petersburg

Nairobi – Viongozi wa Afrika wanalenga kupata majibu kutoka kwa rais wa Urusi, kuhusu mkataba wa kusafirisha nafaka kupitia bahari Nyeusi kutoka Ukraine wakati wa mkutano wao unaoanza leo kule St. Petersburg.

Mbali na swala la usafirishaji nafaka viongozi wa Afrika pia wanatarajiwa kujadili na rais Vladimir Putin hatma ya kundi la Mamluki la Wagner barani Afrika
Mbali na swala la usafirishaji nafaka viongozi wa Afrika pia wanatarajiwa kujadili na rais Vladimir Putin hatma ya kundi la Mamluki la Wagner barani Afrika AP - Ramil Sitdikov
Matangazo ya kibiashara

Mbali na swala la usafirishaji nafaka viongozi wa Afrika pia wanatarajiwa kujadili na rais Vladimir Putin hatma ya kundi la Mamluki la Wagner barani Afrika.

Mkutano wa St Petersburg unajiri siku 10 baada ya rais Putin, kujiondoa katika mktabwa bahari Nyeusi uliowezesha Ukraine kusafirisha nafaka yake kwa dunia licha uvamizi wa Urusi ambao umedumu kwa miezi 17 sasa, rais Putin akituhumu mataifa ya magharibi na Marekani kwa kuhujumu mkataba huo, ambao sasa utasabisha mfumoko wa bei za vyakula.

Marais 49 walitarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa Urusi na Africa ila ni 17 peke ndio wamefika, Urusi ikituhumu mataifa ya magharibi kwa kushiwishi baadhi ya viongozi wa Afrika kususia mkutano huo.

Ni mkutano unaojiri wakati huu Marekani ikituma maafisa wake wa wizara ya fedha kufanya ziara kwa taifa la  Kenya, ambalo rais wake william Ruto amesusia mkutano huo na Somalia, huku waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, akifanya ziara ya tatu barani Afrika tangu Urusi kuvamia nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.