Pata taarifa kuu

Mashambulio ya ndege za kivita yasababisha maafa nchini Sudan

Nairobi – Watu 16 wameuawa jijini Khartoum nchini Sudan baada ya wanajeshi na wanamgambo wa RSF kushambuliana kwa ndege za kivita na makombora hapo jana Jumanne.

Makabilianao yanaendelea kuripotiwa nchini Sudan licha ya wito wa jamii ya kimataifa wa kutaka kusitsihwa kwa mapigano
Makabilianao yanaendelea kuripotiwa nchini Sudan licha ya wito wa jamii ya kimataifa wa kutaka kusitsihwa kwa mapigano AP
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, ripoti kutoka jumuiya ya umoja wa Ulaya, zinasema wakuu wa nchi wanafikiria kutangaza vikwazo zaidi dhidi ya majenerali wawili wanaopigana nchini Sudan, ikiwemo vikwazo vya kusafiri, kuzuia mali zao na akaunti za benki.Haya yanajiri wakatu huu mapigano yakiingia siku ya 100 juma hili.

Wadadisi wa mambo wanasema nyaraka kuhusu mpango huo, zilisambazwa kwa nchi wanachama wiki iliyopita na kwamba itajadiliwa ndani ya siku chache zijazo, mpango huo ukinuwiwa kukamilika kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.

Tayari umoja wa Ulaya umeshatangaza vikwazo kadhaa kwa makampuni na watu wanaohusishwa na kundi la Wagner, ikiwemo operesheni zake nchini Sudan.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, vikwazo hivi vipya, vinatarajiwa kuwa vya juu zaidi kuchukuliwa dhidi ya viongozi wa Sudan, vikitarajiwa kutuma ujumbe mkali kwa jenerali Abdel Fattah al Burhan na mwenzake Mohamed Dagalo.

Katika hatua nyingine Jumuiya ya kimataifa imeonya kuhusu suluhu kuchelewa kupatikana nchini Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.