Pata taarifa kuu

DRC yatia saini mkataba wa madini wa dola bilioni 1.9 na Umoja wa Falme za Kirabu

Umoja wa Falme za Kiarabu Jumatatu ulitia saini mkataba wa dola bilioni 1.9 na kampuni ya uchimbaji madini ya serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ili kuendeleza angalau migodi minne mashariki mwa nchi hiyo inayokumbwa na machafuko, ofii ya rais imebaini.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni mojawapo ya nchi tajiri zaidi kwa madini.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni mojawapo ya nchi tajiri zaidi kwa madini. Getty images/Simon Dawson/Bloomberg
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Rais Félix Tshisekedi ilitangaza katika taarifa Jumatatu jioni kwamba ujumbe kutoka serikali ya Umoja wa Falme za  Kiarabu ulihitimisha ushirikiano huko Kinshasa wenye thamani ya dola bilioni 1.9 na kampuni ya madini ya Kivu na Maniema (SAKIMA). Mkataba huo unatoa fursa ya kuanzishwa kwa "zaidi ya migodi minne ya kiviwanda" katika majimbo ya Kivu Kusini na Maniema, kulingana na taarifa.

Kampuni hii ya serikali, SAKIMA, inamiliki vibali vya uchimbaji madini vyenye bati, tantalum, tungsten na dhahabu. Ofisi ya rais haikueleza ni madini gani yanayohusu mkataba huo. Haya yanajiri baada ya DRC kutia saini mkataba wa miaka 25 na kampuni ya Primera Group ya Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya mauzo ya baadhi ya madini yanayochimbwa kwa njia za kisanaa huko Kivu Kusini.

Chini ya masharti ya mkataba huu, Primera Group ina hisa nyingi katika ubia mbili, Primera Gold kwa dhahabu na Primera Metals kwa "3Ts" (bati, tungsten na tantalum).

DRC inawasilisha mpango huu hasa kama njia ya kupigana dhidi ya usafirishaji wa madini kwa manufaa ya makundi yenye silaha na waasi, ambao ni wengi mashariki mwa DRC. Kinshasa hasa inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 na kupora utajiri wa madini katika eneo hilo, jambo ambalo Kigali inakanusha. Primera Gold ilianza kufanya kazi mwezi Januari huko Kivu Kusini na kufikia mwezi Mei ilikuwa imesafirisha tani moja ya dhahabu iliyoidhinishwa, kulingana na wizara ya fedha ya DRC.

Ripoti iliyochapishwa mwezi Juni na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, hata hivyo, ilitia shaka juu ya uhalali wa migodi ya madini inayosambaza Dhahabu ya Primera. Ripoti hii iliona kuwa inawezekana sana, kwa sababu ya mbinu mbovu za ufuatiliaji, kwamba msururu wa usambazaji unaweza kuchafuliwa na madini kutoka maeneo yanayoodhibitiwa na makundi yenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.