Pata taarifa kuu

Marekani yaongeza vikwazo dhidi ya Wagner na shughuli zake za dhahabu barani Afrika

Marekani imechukuwa vikwazo vipya dhidi ya makampuni na watu binafsi Kusini mwa Jangwa la Sahara. Vikwazo hivi vimechukuliwa hasa kukabilian dhidi ya shughuli haramu ya dhahabu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa manufaa ya kundi la Wagner.

Bendera ya kundi la wanamgambo la Urusi Wagner.
Bendera ya kundi la wanamgambo la Urusi Wagner. © REUTERS / ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Kampuni hy kwanza iliyotajwa ni Midas Resources. Imesajiliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini ni mali ya Incomad (Investment Corporation Madagascar), iliyoanzishwa mwaka wa 2019 kwenye Kisiwa hicho, ambapo Yevgeny Prigozhin mkuu wa Wagner ana ubia wa uchimbaji madini na kampuni ya serikali.

Midas Ressources hata hivyo iliwakilishwa na raia wa Madagascar ilipopata - mwishoni mwa mwaka 2019 - kibali cha uendeshaji wa mgodi wa dhahabu wa Ndassima, unaochukuliwa kuwa mzuri zaidi nchini Madagascar. Kibali ambacho hapo awali kilikuwa kinashikiliwa na kampuni ya Canada ya Axmin, ambayo haikuwahi kutumia eneo hilo kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Tangu wakati huo, Midas Resources, chini ya ulinzi wa mamluki wa Wagner, imetengeneza mgodi huu hii kwa kiasi kikubwa, kwa kutumia minyororo ya ugavi wa nyenzo na uwezo wa kuuza nje wa makampuni mengine yanayohusishwa na Yevgeny Prigozhin.

Kulingana na uchunguzi wa shirika la Bloomberg uliochapishwa siku ya Jumanne: kulingana na picha za satelaiti, Ndassima sasa inaweza kuzalisha zaidi ya tani 4 za dhahabu kila mwaka, au thamani ya karibu dola milioni 290. Shughuli ambayo inakwepa kodi yoyote na ukaguzi na udhibiti wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ndivyo ilivyo kwa kampuni nyingine inayolengwa na Wizara ya Fedha ya Marekani: Diamville, ambayo, kulingana na tafiti kadhaa, inasafirisha almasi za Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kukwepa hati ya kimataifa inayohusishwa na mchakato wa Kimberley, hasa kwa kutumia vyeti vya Cameroon. Diamville, kama vile Midas Resources, pia ilichukuliwa vikwazo na Umoja wa Ulaya mwishoni mwa Februari.

Kampuni nyingine mbili zilizochukuliwa vikwazo ziko nchini Urusi (Limited Liability Company DM) na huko Dubai (Industrial Resources General Trading), na hutumiwa kuchakata bidhaa kwa dola. Jiji kuu la Umoja wa Falme za Kiarabu linazidi kuibuka kuwa kitovu cha ufujaji wa dhahabu na almasi za Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Marekani pia haisahau kuhusika kwa Wagner nchini Mali. Mali za Andrei Nikolaevich Ivanov zimeziwa, anasema mwandishi wetu huko Washington, Guillaume Naudin. Mshirika huyu wa karibu wa Yevgeny Prigozhin, kupitia kampuni ya Africa Politology, anatuhumiwa kujihusisha na biashara ya silaha na, tena, shughuli za uchimbaji madini na maafisa wakuu wa serikali ya Mali. Pia amepigwa marufuku kuingia nchini Marekani.

Je, vikwazo hivi vina nguvu gani?

Vikwazo hivi vinatumika kama ujumbe ulioelekezwa kwa Mataifa, makampuni na watu wanaofanya biashara na kundi la Wagner, na ambao wanaweza kulengwa kwa zamu, lakini swali linazuka kuhusu ufanisi wa vikwazo. Kuanzia mwaka 2020, Wizara ya Fedha ililenga kampuni ya Lobaye Invest, ambayo inadhibiti migodi na misitu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Lakini hii haikuzuia maendeleo ya shughuli za kibiashara za Yevgeny Prigozhin, wala kuanzishwa kwa kituo cha vifaa kwenye bandari ya Douala, nchini Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.