Pata taarifa kuu

IMF imeidhinisha mkopo wa dola bilioni 1.8 kwa Senegal

Nairobi – Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeidhinisha mkopo wa dola bilioni 1.8 kwa nchi ya Senegal kama njia moja ya kusaidia kufufua uchumi wa taifa hilo na kuliepusha kuingia katika majanga mengine.

Mkopo huo unalenga kuisaidia nchi hiyo kuimarisha uchumi wake ulioharibika kutokana na uviko 19 na vita vya Ukraine
Mkopo huo unalenga kuisaidia nchi hiyo kuimarisha uchumi wake ulioharibika kutokana na uviko 19 na vita vya Ukraine REUTERS - JOHANNES CHRISTO
Matangazo ya kibiashara

Taifa hilo la Afrika Magharibi litapokea malipo ya awali ya takriban $216m, IMF ilisema katika taarifa yake Jumatatu kufuatia mkutano wa bodi kuu.

Mkopo huo wa miaka mitatu pia unalenga kupiga jeki juhudi za Senegal kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

IMF katika taarifa yake inasema kuwa vita vya Urusi na Ukraine vilizuia kuimarika kwa uchumi ambao ulikuwa umesambaratika kutokana na makali ya uviko 19.

Hata hivyo inakadiria kiwango cha ukuaji cha 8.3% katika mwaka wa 2023 wakati uzalishaji wa mafuta na gesi unapoanza nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.