Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

unisia: Ofisi ya Mwendesha Mashtaka yapinga kuachiliwa kwa Chaïma Issa

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tunisia Chaïma Issa, ambaye kuachiliwa kwake kuliamriwa na jaji siku ya Ijumaa, hatimaye atasalia gerezani baada ya upande wa mashtaka kukataa uamuzi wa kumwachilia huru, mawakili wake wamesema.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Tunisia, Tunis. Mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na ya kimataifa yameshutumu kukamatwa kwa wanasiasa hao, yakichukizwa na utashi wa kisiasa "kukandamiza sauti huru".
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Tunisia, Tunis. Mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na ya kimataifa yameshutumu kukamatwa kwa wanasiasa hao, yakichukizwa na utashi wa kisiasa "kukandamiza sauti huru". © Éric Bataillon/RFI
Matangazo ya kibiashara

Jaji katika mahakama ya kukabiliana na ugaidi ameamuru kuachiliwa kwa Chaïma Issa, anayezuiliwa tangu mwezi Februari kwa tuhuma za "njama dhidi ya usalama wa taifa", lakini rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka imesimamisha utekelezaji wa uamuzi huu, wameelezea mawakili wa mwanasiasa huyo wa upinzani. Alipokamatwa Februari 22, Chaïma Issa, 43, ni mmoja wa vigogo wa National Salvation Front (FSN), muungano mkuu wa upinzani dhidi ya Rais Kais Saied ambaye alichukua mamlaka kamili nchini Tunisia mnamo Julai 25, 2021.

"Uamuzi wa kumwachilia Chaïma Issa ni wa kisiasa, haukuwa uamuzi wa uhuru wa jaji wa uchunguzi. Wamekata rufaa, kwa nini? Sijui lakini pia ni wa kisiasa", amesema kiongozi wa FSN Ahmed Nejib Chebbi. Jaji wa mahakama ya kupambana na ugaidi "yuko chini ya amri", ameongeza.

Bi. Issa alikamatwa pamoja na wanasiasa wengine wa upinzani ishirini na watu wengine kutoka jumuiya za wafanyabiashara na vyombo vya habari kama sehemu ya uchunguzi wa "njama dhidi ya usalama wa taifa". Rais Saied aliwataja waliokamatwa kuwa ni "magaidi". Baadhi walihojiwa kuhusu mikutano yao na mawasiliano ya simu na wanadiplomasia wa kigeni, wengine kuhusu mahojiano waliotoa kwa vyombo vya habari, kulingana na wanasheria wao.

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na ya kimataifa yameshutumu kukamatwa kwa wanasiasa hao, yakichukizwa na utashi wa kisiasa "kukandamiza sauti huru". Mnamo Juni 16, Bw. Chebbi alimshutumu Bw. Saied kwa kutaka "kukandamiza" aina yoyote ya upinzani, kabla ya kuhojiwa katika kitengo cha kupambana na ugaidi kama sehemu ya uchunguzi wa "njama dhidi ya usalama wa 'Nchi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.