Pata taarifa kuu

Kenya: Ruto atoa wito kwa kuangaziwa upya kwa madeni ya Afrika

Nairobi – Rais wa Kenya, William Ruto, amesema haikubaliki kuona baadhi ya mataifa yenye nguvu, yanatumia taasisi za kimataifa za kifedha kuzinyonya nchi zinazoendelea kupitia mikopo.

Rais wa Kenya William Ruto, Machi 28, 2023
Rais wa Kenya William Ruto, Machi 28, 2023 © REUTERS/Michele Tantussi
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika kongamano la jijini Paris, rais Ruto, amesema wakati ufike kwa nchi za Afrika kulipa gharama zinazohitajika kwenye taasisi hizo ili na wao waweze kufanya maamuzi.

Rais Ruto ameiomba Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kupunguza sheria kali za mikopo inayotolewa kwa nchi za Afrika ili kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali kwa haki.

Ruto alitoa wito huu alipokutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, mkuu wa IMF Kristalina Georgieva, na rais wa  Benki ya Dunia Ajay Banga mjini Paris Alhamisi ambapo pia aliwataka viongozi wa dunia wanaohudhuria Mkutano wa New Global Financial Pact Summit kuunga mkono wito wake.

Serikali ya rais Ruto ilipokea $600m (£470m) kutoka kwa shirika la IMF mwaka wa  2022.

Pia ilipata $993m kutoka Benki ya Dunia mwezi Mei kusaidia serikali kufadhili bajeti yake.

Nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na changamoto za madeni makubwa kutoka kwa wakopeshaji wa nje.

Kwa muda sasa nchi za Afrika zimeyanyooshea kidole baadhi ya mataifa yenye nguvu, kujilimbikizia mamlaka katika taasisi za kimataifa za kifedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.