Pata taarifa kuu

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anapendekeza 'kuundwa upya' ujumbe nchini Mali

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kujadili hali ya Mali siku ya Ijumaa, kabla ya upigaji kura uliopangwa kufanyika Juni 29 kuhusu taratibu za kuongeza muda ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali kwa mpango wa bajeti ya mwaka ya dola bilioni 1.2, kipindi ambacho kinamalizika tarehe 30 Juni.

"Ni muhimu sana kwamba uchunguzi wa kuaminika na wa uwazi ufanyike bila kuchelewa ili wahusika wa vitendo hivi waweze kujibu," amesema Antonio Guterres.
"Ni muhimu sana kwamba uchunguzi wa kuaminika na wa uwazi ufanyike bila kuchelewa ili wahusika wa vitendo hivi waweze kujibu," amesema Antonio Guterres. AP - Khalil Senosi
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amependekeza siku ya Jumanne kwa Baraza la Usalama "kuunda upya" ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), ili kuuimarisha, pamoja na idadi ya wafanyakazi wa mara kwa mara, kwenye idadi ndogo ya "vipaumbele" ili kuufanya kuwa na ufanisi zaidi.

Baraza hilo linatazamiwa kujadili hali ya Mali siku ya Ijumaa, kabla ya upigaji kura uliopangwa kufanyika Juni 29 kuhusu taratibu za kuongeza muda ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali kwa mpango wa bajeti ya mwaka ya dola bilioni 1.2, kipindi ambacho kinamalizika tarehe 30 Juni.

"Wakati hakuna shaka kwamba Mali inaingia katika kipindi muhimu cha kurejea kwa utaratibu wa kikatiba, kuendelea kuwepo kwa MINUSMA kunasalia kuwa muhimu," amesema Antonio Guterres katika ripoti yake iliyochapishwa siku ya Jumanne.

Lakini "hali iliyopo sio na haiwezi kuwa chaguo, wala kwa watu wa Mali, ambao wanaendelea kuteseka na ghasia zisizoelezeka na ambao hamu yao ya kuwa na maisha bora ya baadaye bado haijatimizwa, wala kwa jumuiya ya kimataifa, ambayo tangu mwaka 2013, imekuwa ikiwekeza kwa kiasi kikubwa katika kuleta utulivu wa nchi."

Katika muktadha huu, Katibu Mkuu anapendekeza kwa Baraza la Usalama kuongeza muda wa MINUSMA kwa mwaka mmoja, huku ikidumisha idadi ya wafanyakazi walioidhinishwa katika ngazi yao ya sasa (askari 13,289 na maafisa wa polisi 1,920) - idadi ambayo leo iko chini (askari 11,102 na maafisa wa polisi 1,315 hadi Mei 23), wakati ni vigumu kupata nchi zinazochangia wanajeshi na nyingi zimetangaza kujiondoa.

Lakini "Ninakusudia kutumia mamlaka yangu kupanga upya misheni na kupeleka wafanyakazi kutoka sehemu ya kiraia na sehemu ya wafanyakazi waliovaa sare hadi pale wanapohitajika zaidi, kulingana na maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mkataba (kwa ajili ya amani na maridhiano) na mpito wa kisiasa,” amesema.

Kwa hivyo, anapendekeza kwa Baraza "kurekebisha kazi za MINUSMA karibu na vipaumbele vichache ili kuboresha ufanisi wake wa jumla hadi mwisho wa mpito wa kisiasa, uliopangwa mwezi Machi 2024".

'Matatizo magumu'

Mnamo mwezi Januari, kwa ombi la Baraza la Usalama, Antonio Guterres ametoa tathmini ya kimkakati ya ujumbe ulioundwa mnamo mwaka 2013 kusaidia kuleta utulivu hali inayotishiwa na kuanguka chini ya msukumo wa wanajihadi, kulinda raia, kuchangia juhudi za amani, kutetea haki za binadamu...

Huku hali ya usalama ikizidi kuwa mbaya na walinda amani wakilengwa mara kwa mara, aliweka chaguzi tatu mezani, kutoka kwa ongezeko la wanajeshi hadi kuondolewa kwa jumla kwa wanajeshi ikiwa masharti muhimu hayatatimizwa.

Chaguo la kati analopendekeza siku ya Jumanne linaweza kuhusisha hasa kufungwa kwa baadhi ya kambi, kama vile ile ya Ber katika eneo la Timbuktu, na "kujiondoa kwa uratibu" kutoka kwa baadhi ya maeneo katika eneo la Kidal.

Katibu Mkuu anabainisha kuwa "mamlaka za Mali zimefahamisha mara kadhaa kwamba hakuna chaguo lililopendekezwa linalokidhi matarajio au vipaumbele vya raia wa Mali".

Miongoni mwa masharti muhimu ya kuamua masharti ya kudumisha ujumbe huo, Antonio Guterres alisisitiza mwezi Januari juu ya maendeleo ya mpito wa kisiasa ambao hutoa, baada ya mapinduzi mawili ya kijeshi, kurejea kwa raia madarakani Machi 2024, pamoja na uhuru wa harakati za walinda amani.

"Katika miezi ya hivi karibuni, hali nchini Mali, kutoka kwa mtazamo wa vigezo hivi, imepata mabadiliko tofauti," amesema siku ya Jumanne.

Kwa upande mwingine, anabainisha "kwa wasiwasi mkubwa" mahitimisho ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, ambayo mwezi Mei ilishutumu jeshi la Mali na wapiganaji "wa kigeni" kwa kuwaua watu wasiopungua 500 Machi 2022, wakati wa operesheni dhidi ya wanajihadi huko Moura.

"Ni muhimu sana kwamba uchunguzi wa kuaminika na wa uwazi ufanyike bila kuchelewa ili wahusika wa vitendo hivi waweze kujibu," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.