Pata taarifa kuu
USALAMA-ELIMU

Niger: Zaidi ya shule 900 zafungwa kwa sababu ya ukosefu wa usalama Tillabéri

Zaidi ya shule 900 zimefungwa kwa sababu ya ukosefu wa usalama huko Tillabéri kusini-magharibi mwa Niger. Hii ni takwimu iliyotolewa na Waziri wa Elimu wa Niger kufuatia ziara ya mwishoni mwa mwezi wa Mei katika eneo hili ambalo linalengwa mara kwa mara na mashambulizi ya wanajihadi. Serikali ya Niger inasema inafanya kila iwezalo kuhakikisha uendelevu wa elimu. Walimu wanaomba ulinzi uimarishwe ili waweze kuendelea kufanya kazi.

Kutokana na mashambulizi ya wanajihadi, mamia ya shule zimefungwa katika eneo la Tillabéri kusini magharibi mwa Niger.
Kutokana na mashambulizi ya wanajihadi, mamia ya shule zimefungwa katika eneo la Tillabéri kusini magharibi mwa Niger. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa maeneo ya ukosefu wa usalama pia yametambuliwa katika mikoa ya Diffa, Maradi na Tahoua, ni katika Tillabéri ambako matatizo ni makubwa zaidi kwa wanafunzi wa shule. Mwishoni mwa mwezi wa Mei, zaidi ya shule 900 hazikurudi kufanya kazi tena katika eneo hili la mpaka wa Mali na Burkina Faso.

Kulingana na Waziri wa Elimu wa Niger, 18% ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hawaendi tena shule huko Tillabéri, sawatakriban wanafunzi 79,000, kati ya 438,000 katika eneo hilo. Hii ni asilimia kubwa sana, anabaini Ibrahim Natatou, licha ya juhudi ambazo Serikali inahakikisha kupeleka, kupitia shule za mapokezi, vituo zinazowakusanya wanafunzi, migahawa ya dharura kwa wanafunzi kwa mfano.

Shule inapofungwa, baadhi ya wanafunzi huenda shule nyingine, lakini wengine huacha shule kwa kukimbia, anaelezea katibu mkuu wa Muungano wa kitaifa wa Walimu nchini Niger, SNEN. Walimu pia wana hofu, anaongeza Laouali Issoufou, ambaye anaomba kuwepo na doria zaidi za kijeshi, lakini pia msaada wa kifedha. SNEN pia inataka marekebisho mahususi kwa programu na ratiba katika maeneo yenye migogoro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.