Pata taarifa kuu

Uganda: Rais Museveni atia saini sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja

NAIROBI – Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini, mswada unaopinga vitendo vya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, baada ya kufanyiwa marekebisho na wabunge.

Rais Museveni atia saini sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja
Rais Museveni atia saini sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja © SERIKALI YA UGANDA
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya rais Museveni inakuja licha ya mataifa ya Magharibi na wanaharakati wa haki za binadamu kumtaka kutosaini mswada huo kwa misingi kuwa unakiuka haki za binadamu.

Mswada huo ulipitishwa kwa mara ya kwanza na bunge nchini humo mwezi Machi kabla ya kurejeshwa tena bungeni kwa marekebisho.

Watu wanaojihusisha na ushoga nchini humo sasa watafungwa maisha jela iwapo watashtakiwa.

Sheria pia inaeleza adhabu ya kifo kwa makosa yaliyokithiri, katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mtoto mdogo, mlemavu au ambapo mwathirika wa unyanyasaji ameambukizwa na ugonjwa wa maisha.

Raia katika taifa hilo la Afrika Mashariki pia wametakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka kuhusu visa vya ushoga vinavyotekelezwa dhidi ya watoto au watu wanaoishi na changamoto za kimaumbile.

Hapo awali sheria ilihalalisha kuwatambua watu wachache wa jinsia moja lakini Museveni alisema kuwa hilo lingesababisha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa watu kwa sababu ya muonekano wao tu.

Baadhi ya mataifa ya Afrika kama vile Uganda yameharamisha mapenzi ya jinsia moja
Baadhi ya mataifa ya Afrika kama vile Uganda yameharamisha mapenzi ya jinsia moja AP

Kifungu hiki kiliondolewa wakati rais aliporudisha mswada huo bungeni. Kuna uwezekano kwamba sheria hiyo itapingwa mahakamani.

Mswada sawa na huo ulitupiliwa mbali na mahakama ya kikatiba ya Uganda mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.