Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mapigano yaendelea nchini Sudan, licha ya ahadi ya makubaliano mapya

Usitishaji vita wa wiki moja unatakiwa kuanza kutekelezwa Jumatatu jioni kati ya jeshi na wanamgambo wanaowania mamlaka nchini Sudan na wanaendelea, kwa sasa, mapigano yao makali.

Mapigano yanaendelea kurindima katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Mapigano yanaendelea kurindima katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili wapatanishi ambao ni Marekani na Saudi Arabia walitangaza kwamba wamepata, baada ya wiki mbili za mazungumzo nchini Saudi Arabia, wameweza kuafikiana na pande hasimu kusitisha mapigano kwa wiki moja kuanzia Jumatatu saa moja na dakika 45 usiku (sawa na saa tatu na dakika 45 usiku saa za Afrika ya Kati).

Kambi hizo mbili zimetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba zinataka kuheshimu mapatano haya, ambayo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, IGAD, wamekaribisha hatu hiyo. Lakini katika zaidi ya wiki tano za vita, makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano yalitangazwa na kukiukwa mara moja.

"Hatuna imani na ahadi hizi: kila wakati, wanatangaza kusitisha mapigano na kuanza tena mapigano yao mara moja," anasema Adam Issa, mfanyabiashara kutoka Darfur, eneo la magharibi mwa nchi lililoathirika zaidi na mapigano na vikosi vya Khartoum.

"Jambo muhimu zaidi si kutangaza mapatano lakini kuheshimu na kudhamini eneo salama kwa ajili ya chakula na misaada," ameongeza mkazi mwingine wa Khartoum.

Tangu Aprili 15, vita kati ya jeshi la Jenerali Abdel Fattah al-Burhane na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (FSR), wanaoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu katika nchi hii ya Afrika Mashariki, nchi maskini zaidi duniani, ambapo zaidi ya watu milioni moja wamekimbia makazi yao.

Tangu kuanza kwa vita, majenerali hao wawili wamekuwa wakichunguzana kupitia vyombo vya habari, lakini hawajazungumza tangu tangazo hili.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, anatarajiwa kuhutubia Baraza la Usalama leo Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.