Pata taarifa kuu

Mamia ya Raia wa Togo wajitokeza kujisajili kama wapiga kura.

Nairobi – Vituo vya usajili wa upigaji kura vilifunguliwa mapema leo na ndani ya saa chache watu walionekana kumiminika ili kusajiliwa.Uchaguzi wa mitaa na bunge unatarajiwa kufanyika mwezi wa 12  mwaka huu.

Foleni ya Raia wa Togo waliojitokeza kupiga kura mwaka 2013
Foleni ya Raia wa Togo waliojitokeza kupiga kura mwaka 2013 Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Katika shughuli hiyo ya usajili kuna baadhi ya changamoto zimeshuhudiwa kama vile wengine kukosa kusajiliwa kwasabababu ya uhaba wa karatasi za usajili na hata tarakilishi kutofanya kazi.

"Ni ngumu kidogo, kusema ukweli, kwa sababu mambo hayaendi vizuri. Wanasema kwamba karatasi zimekamilika, mashine hazifanyi kazi. Hakuna ila mabishano. Unaona, haisongi," Sarath Sidibe, ambaye ni mpishi alisema kutoka kituo kilichoko katika mji mkuu wa Lome.

Katika jaribio lake la pili Komlan Edoh, seremala, alifanikiwa zaidi “Jana nilikuwepo lakini kwa vile watu walikuwa wengi na nina mambo mengine ya kuhangaikia ndiyo maana niliondoka lakini leo nimekuja saa sita imekwenda vizuri nikapokea kadi yangu,” alisema. .

Evariste Toganou, ambaye anafanya kazi katika duka kubwa, alionekana kukosa subira. "Nitachukua kadi yangu ya mpiga kura bila kujali shida. Kwa sababu wakati huu, lazima nipige kura."

Kama wapiga kura wengi wa 2018 Toganou alikataa kupiga kura baada ya vyama vikuu vya upinzani kuwataka watu kususia uchaguzi wa wabunge.

Lakini wakati huu, wamekuwa wakiwahimiza wafuasi wao kujitokeza kwa nguvu.

Lakini ikiwa kila mtu anayetaka kupiga kura ataweza kujiandikisha sina uhakika kwani maafisa wa uchaguzi wanakiri kuwa wanatatizika.

"Tumezidiwa sana, lakini sawa. Tunajaribu kukabiliana nayo, lazima tufanye kila tuwezalo kujaribu kudhibiti kila mtu aliye hapa," Kokouvi Paul Dobe kutoka Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi alisema.

Mnamo mwaka wa 2018, chama cha Rais Faure Gnassingbé ,kilipata wingi wa viti 59 kati ya 91 vya Bunge la Kitaifa, huku viongozi wa muungano mkuu wa vyama 14 vya upinzani wakisusia uchaguzi.

Walikasirika baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mgogoro mkubwa wa kisiasa na maandamano kadhaa, ambayo yalikandamizwa vikali, dhidi ya mageuzi yanayomruhusu rais kugombea tena uchaguzi wa 2020 na 2025.

Ni wazi kuwa watu wengi kati ya milioni nane wa Togo wanataka mabadiliko.

Sio tu kwamba nchi yao inasalia kuwa maskini, kama sehemu kubwa ya eneo la Sahel pia sasa inakumbwa na mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali.

Na familia hiyo hiyo imekuwa madarakani kwa miaka 56.Gnassingbé amekuwa rais tangu 2005 na kabla yake ni babake Gnassingbé Eyadéma ambaye alichukua mamlaka mnamo 1967.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.