Pata taarifa kuu

Afrika Kusini haijiondoi ICC, yalaumu dosari ya mawasiliano

Ofisi ya rais wa Afrika Kusini, imesema kuwa matamshi ya rais Cyril Ramaphosa yalieleweka visivyo, na kwamba nchi hiyo inasalia mwanachama wa mahakama hiyo.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Phill Magakoe / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais imesema, mawasiliano kutoka chama tawala cha ANC, yalikuwa na dosari.

Hii ni baada yake hapo jana, rais Ramaphosa kusema kuwa chama hicho kimefanya maamuzi ya kujiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC, ambayo mwezi uliopita ilitoa kibali cha kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladmir Putin.

Wakili Jebra Kambole akiwa nchini Tanzania, amezungumza na RFI Kiswahili, kuhusu misimamo hii tofauti.

Afrika Kusini kuwa na msimamo wa kuyumbayumba juu ya ICC, ni katika muendelezo ule ule wa nchi za kiafrika, kutokuwa na uwajibikaji na kutoheshimu sheria za kimataifa,” Amesema wakili Jebra.
00:35

Jebra Kambole kuhusu matamshi tata ya Afrika Kusini kujiondoa ICC

Kibali hiki cha kukamatwa kwa Putin, kinamaanisha kuwa Afrika Kusini –ambayo itakuwa mwenyeji wa kongamano la mataifa ya BRICS ikiwemo Brazil, Russia, India, China na South Africa – itamkamata Putin atakapowasili nchini humo baadaye mwaka huu.

Hapo wali chama cha ANC, kiliwaambia waandishi wa habari kuwa nchi hiyo kujiondoa katika mahakama ya ICC, ni swala ambalo liliibuliwa katika mkutano wa baraza la chama hicho wikendi iliyopita.

ICC ilitoa kibali hicho kutokana na madai kuwa utawala wa Kremlin, uliwarejesha nyumbani watoto wa Ukraine kinyume cha sheria.

Kuhusu iwapo Afrika Kusini itamkamata Putin au la, Ramaphosa alisema suala hilo linatathminiwa, lakini awali, katibu mkuu wa ANC Fikile Mbalula alitangaza kuwa Putin anaweza kutembelea nchi hiyo wakati wowote.

Ramaphosa ambaye mwaka 2022 alilaumu NATO kwa vita vinavyoendelea Ukraine, amesema anaheshimu uamuzi wa hivi punde wa Finland wa kujiunga na muungano huo, matamshi aliyoyatoa wakati wa ziara ya rais wa Finland nchini humo Sauli Niinistô, kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.