Pata taarifa kuu

Rais: ANC imeamua kuwa Afrika Kusini ijiondoe ICC

NAIROBI – Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amesema chama cha African National Congress, ANC,  kimefikia makubaliano kuwa nchi hiyo, ijiondoe katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati wa hotuba yake kwa wabunge Februari 10, 2022 katika Ukumbi wa Jiji la Cape Town.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati wa hotuba yake kwa wabunge Februari 10, 2022 katika Ukumbi wa Jiji la Cape Town. © AP/Nic Bothma
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya ICC yenye makao yake makuu nchini Uholanzi, mwezi uliopita, ilitoa kibali cha kukamatwa dhidi ya rais wa Urusi Vladmir Putin, ikimaanisha kuwa Pretoria ingemzuia rais huyo, iwapo atahudhuria kongamano linaloandaliwa nchini humo baadaye mwaka huu.

Kongamano hilo linawaleta pamoja marais kutoka Brazili, Urusi, India, China na Afrika Kusini.

Ndiyo, chama tawala...kimechukua uamuzi huo kwamba ni jambo la busara kwamba Afrika Kusini inapaswa kujiondoa katika ICC, Ramaphosa amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa pamoja na Rais wa Ufini Sauli Niinisto.

Rais Ramaphosa amesema uamuzi huo unajiri baada ya mkutano ulioandaliwa na chama tawala ANC wikendi iliyopita, na uamuzi huo ulifikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya kile kinachoonekana kama unyanyasaji wa mahakama kwa nchi fulani.

Tungependa suala hili la kutotendewa haki lijadiliwe ipasavyo, lakini kwa sasa chama tawala kimeamua kwamba nchi ijiondoe, amesema Ramaphosa.

Kibali hicho cha kukamatwa dhidi ya Putin kilitolewa kutokana na madai kuwa utawala wa Kremlin uliwarejesha nyumbani kinyume cha sheria watoto wa nchini Ukraine.

Kuhusu suala la iwapo Afrika Kusini itamkamata Purin, rais Ramaphosa amesema jambo hilo linaendelea kutathminiwa, lakini katibu mkuu wa chama hapo awali, alikuwa ametangaza kuwa Putin anaweza tembea nchini humo wakati wowote.

Uhusiano na Moscow

Utawala wa Pretoria una uhusiano wa karibu na Moscow, tangu Kremlin iunge mkono chama cha ANC katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Tangu Urusi kuivamia Ukraine, Afrika Kusini, haijajitokeza wazi kulaani kitendo hicho, ikisema haitaki kuchukua upande wowote na inaunga mkono majadiliano ili kumaliza mzozo uliopo.

Ramaphosa amesema amewasiliana na Putin mara kwa mara kwenye simu, na ujumbe wake umekuwa haja ya mazungumzo.

Kujiondoa ICC

Hii sio mara ya kwanza nchi ya Afrika Kusini kutaka kujiondoa katika mahakama ya ICC.

Mwaka 2016, ilifanya jaribio hilo kutokana na mzozo wa mwaka mmoja kabla, wakati rais wa zamani wa Sudan, Omar al-Bashir, alizuru nchi hiyo, kuhudhuria kongamano la Umoja wa Afrika.

Utawala wa Pretoria ulikataa kumkamata licha ya kibali cha kukamatwa dhidi yake, akihusishwa na madai ya uhalifu wa kivita.

Uamuzi huo wa kujiondoa ulikataliwa, mahakama ya ICC ikisema kufanya hivyo itakuwa kinyume cha sheria zinazoiongoza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.