Pata taarifa kuu

Mali: kundi la Islamic State linadhibiti mji wa Tidermène

NAIROBI – Nchini Mali, kundi la Islamic State linadhibiti mji wa Tidermène, umbali wa Kilomita 75 Kaskazini mwa jimbo la Menaka, karibu na nchi jirani ya Niger.

Makundi ya kijihadi yamekuwa yakihangaisha usalama wa raia wa Mali kwa muda sasa
Makundi ya kijihadi yamekuwa yakihangaisha usalama wa raia wa Mali kwa muda sasa Souleymane AG ANARA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu siku ya Jumatatu mji huo  ulivamiwa na kundi hilo kwa mujibu wa waakazi. Hii imekuja pia baada ya kundi hilo pia kuuzingira mji wa Menaka, na kuwazidi wapinzani wao JNIm wanaofungana na kundi la Al Qaeda.

Kuendelea kudhibiti miji hiyo miwili, inamaana kuwa makundi hayo yanaendelea kuligawa taifa hilo na kwa lengo la kutawala eneo la Kaskazini.

Maelfu ya watu wameendelea kuhofia maisha yao na kuyakimbia makwao, wengi wakiamua kuhamia katika mji wa Menaka, huku idadi ya wakimbizi ikielezwa kuongezeka kutoka Elfu 11  hadi elfu 30 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Jeshi la Umoja wa Mataifa MINUSMA linasema licha ya makundi hayo kuchukua maeneo zaidi hali ni utulivu.

Mwezi Desemba mwaka uliopita, makundi yenye silaha yaliyokuwa yametia saini mkataba wa amani na serikali, yalijiondoa kwenye makubaliano hayo, yakiishtumu uongozi wa Bamako kwa kutoonesha utashi  wa kisiasa.

Kwa sasa jitihada za Kimataifa, chini ya Umoja wa Mataifa zinaendelea kwa makundi hayo na serikali ya Mali, kutekeleza mkataba wa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.