Pata taarifa kuu

DRC yapoteza dola bilioni moja kwa mwaka kutokana na usafirishaji haramu wa madini

Usafirishaji wa madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeorodheshwa kwenye ripoti mbalimbali zisizo za kiserikali na Umoja wa Mataifa. Kulingana na Wizara ya Fedha ya Marekani, zaidi ya asilimia 90 ya Dhahabu inayozalishwa nchini DRC inasafirishwa kwa njia ya magendo kupitia nchi jirani, hususan Rwanda na Uganda.

Kinshasa inaamini kuwa nchi jirani ya Rwanda ndiyo mnufaika mkuu wa ulanguzi wa madini kutoka DRC.
Kinshasa inaamini kuwa nchi jirani ya Rwanda ndiyo mnufaika mkuu wa ulanguzi wa madini kutoka DRC. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepoteza faida ya tani za Dhahabu, lakini pia za Tungsten, Tantalum, au Bati  kwa sababu ya usafirishaji haramu wa madini mashariki mwa nchi. Upungufu ambao Waziri wa Fedha wa Kongo, Nicolas Kazadi, alikadiria, katika mahojiano na Gazeti la Financial Times mapema wiki hii, kuwa dola bilioni moja kwa mwaka. Na kwa upande wa pili, nchi jirani ya Rwanda itakuwa mnufaika mkubwa wa biashara hii.

"Ni vigumu kujua ni kiasi gani inavuka njia zisizo halali, anaeleza Jacques Mukena, mtaalamu wa utawala na uchumi katika Taasisi ya Kongo ya Utafiti wa Siasa, Utawala na Vurugu. Haya ni makadirio tu kulingana na mauzo ya nje kutoka Rwanda na Uganda. Kwa kweli, nchini DRC hakuna kiwanda cha kusafisha dhahabu, lakini kuna kiwanda cha kusafisha dhahabu nchini Rwanda na Uganda. Ni kwa msingi wa mauzo ya viwanda hivi ambapo kunaweza kupelekea kujua zaidi au chini ya kiasi ambacho nchi hizi mbili zinauza nje. Hii hailingani na uzalishaji wao wa ndani. Huu ni upungufu wa kweli kwa DRC, anathibitisha mtaalam.

Ushirikiano na Umoja wa Falme za Kiarabu

Ili kukabiliana na mauzo haramu ya Dhahabu, mamlaka ya Kongo ilishirikiana na Falme za Kiarabu na kuunda Primera Gold DRC. Madhumuni ya ubia: kunasa rasmi madini ya thamani yaliyotolewa katika mkoa wa Kivu Kusini. “Primera Gold inanunua dhahabu moja kwa moja kutoka kwa wachimbaji wadogo walioko DRC na kuisafirisha kwenda Umojawa Falme za Kiarabu. Ili kuifanya iwe rasmi zaidi na pia isipitie tena au isitegemee tena Rwanda na Uganda, anasisitiza Jacques Mukena. Na Primera Gold itarasimisha hilo. »

Siku chache zilizopita, Waziri wa Fedha alitangaza kuwa Primera Gold DRC imeruhusu mauzo ya zaidi ya kilo 450 za Dhahabu tangu kuzinduliwa kwake mwezi Januari dhidi ya kilo 34 rasmi mwaka jana.

Rais Kagame akanusha kuhusika kwa Rwanda

Katika mkutano wake wa mwisho, mwanzoni mwa mwezi Machi, Rais Kagame kwa mara nyingine tena alikanusha kuunga mkono wizi wa madini unaofanywa na M23 nchini DRC. "Hizi ni hadithi zisizo na maana za kuwaondoa watu kutoka kwenye tatizo halisi," alisema, akihalalisha hasa kwamba nchi yake ilikuwa na rasilimali zake kwa Dhahabu na Coltan, kwa mfano.

Tayari chini ya vikwazo vya Marekani, Alain Goetz, mkuu wa kiwanda cha kusafisha dhahabu nchini Uganda, aliongezwa kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya mwishoni mwa mwaka. Anatuhumiwa kujinufaisha kutokana na mzozo wa silaha mashariki mwa DRC na kujihusisha na biashara haramu ya madini ya Dhahabu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.