Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Shule zalazimika kufunga kutokana na ghasia za wanajihadi nchini Burkina Faso

Takriban shule moja kati ya nne imefungwa nchini Burkina Faso kutokana na ghasia za wanajihadi ambazo zimeikumba nchi hiyo tangu mwaka 2015 na zimekuwa zikiongezeka kwa miezi kadhaa, shirika lisilo la kiserikali la Norway limesema katika taarifa yake leo Jumanne.

Shule ya msingi katika eneo la Dourtenga, Burkina Faso.
Shule ya msingi katika eneo la Dourtenga, Burkina Faso. Β© KKB by Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwezi Februari, shule 6,134 zilifungwa, ongezeko la zaidi ya 40% tangu mwezi Mei 2022, linabainisha shirika lisilo la kiserikali la Norwegian Refugee Council (NRC). "Zaidi ya watoto milioni moja nchini Burkina Faso wameathiriwa" na kufungwa kwa shule, "mara nyingi wakiumizwa na kuhama makazi yao na migogoro ya kila mara", NRC imeongeza.

"Ni robo tu ya watoto walioathiriwa wamepangiwa madarasa mapya. Wengi wao hawajapata fursa ya kusoma tena," anasema mkurugenzi wa NRC nchini Burkina Faso, Hassane Hamadou, kinukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari. Anatoa wito kwa mamlaka ya nchi na mashirika yanayotoa misaada ya kibinadamu "kuongeza juhudi zao", "kama jambo la dharura".

Mtoto anapokuwa hayuko shuleni, yuko katika hatari zaidi ya kutumikishwa, kuwa mwathiriwa wa ghasia na usafirishaji haramu wa binadamu, na hata kusajiliwa na makundi yenye silaha," amesema mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini  ​​​​Burkina Faso, Sandra Lattouf, pia akinukuliwa na NRC.

Burkina Faso ina "karibu nusu ya shule zilizofungwa katika Afrika ya Kati na Magharibi", kulingana na NCR. Shirika hili linasema nchi jirani za Mali na Niger zina 1,762 na 878. 3,285 zimefungwa nchini Cameroon, 1,344 nchini DRC, 181 nchini Nigeria, 134 nchini Chad na 13 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

NRC inaaini kwamba idadi ya shule zilizofungwa nchini Burkina Faso ni kubwa zaidi katika mikoa ya Boucle du Mouhoun (magharibi), Sahel na mkoa wa Mashariki, mikoa inayolengwa mara kwa mara na mashambulizi. Maeneo haya pia yameathiriwa na uhaba wa chakula, 'moja ya sababu za watot kuacha shule", kulingana na Yembuani Yves Ouoba, mkurugenzi wa shirika la Tin Tua kutoka nchini Burkina Faso.

Hali hii inawaathiri walimu 31,000, kati yao 6,300 wamepangiwa shule nyingine. NCR inatambua, hata hivyo, kwamba "kufungua upya" na "kuhamishwa" kwa shule tangu mwezi Januari "kunachukua hatua katika mwelekeo sahihi".

Burkina Faso, imekumbwa na ghasia za wanajihadi tangu 2015 ambazo zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 10,000 na wengine milioni mbili kuwa wakimbizi wa ndani. Mwezi Machi, UNICEF ilionyesha kuwa watoto milioni 10 walitishiwa na ukosefu wa usalama katikati mwa Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.