Pata taarifa kuu

Zaidi ya shule 5,700 zafungwa nchini Burkina Faso kutokana na ukosefu wa usalama

Nchini Burkina Faso, ukosefu wa usalama umesababisha kufungwa kwa zaidi ya shule 5,700, kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka Sekretarieti ya Kiufundi ya Elimu ya Dharura, ambayo iko chini ya mamlaka ya Wizara ya Elimu.

Shule ya msingi huko Dori, mji ulio kaskazini mashariki mwa Burkina Faso, unaokumbwa na tishio la wanajihadi.
Shule ya msingi huko Dori, mji ulio kaskazini mashariki mwa Burkina Faso, unaokumbwa na tishio la wanajihadi. OLYMPIA DE MAISMONT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watoto milioni moja wameathiriwa na kufungwa kwa shule. Miongoni mwao, wengi wameweza kujiandikisha tena katika shule zingine, kulingana na Wizara ya Elimu, ambayo bado inahesabu watoto 51,000 ambao hawajaenda shule. Na shinikizo kwa shule zinazofanya kazi inakuwa ngumu kuhimili.

Katika eneo la Sahel, Mashariki au Boucle du Mouhoun, walimu wamekuwa walengwa wa watu wenye silaha, anaelezea Koudougou Robert Kaboré, katibu mkuu wa chama cha waalimu. “Miongoni mwa wawakilishi wa Serikali, wazee wamefukuzwa. Wengi wameuawa, hata wanafunzi, ameongeza katibu mkuu wa chama cha waalimu. Mafundisho ya lungha ya Kifaransa, kundi la kigaidi halitaki. Hali ambayo inazua utata. Kulingana na wizara hiyo, karibu walimu 29,000 wameathiriwa na ukosefu huo wa usalama.

Watoto wanaoishi katika mazingira magumu

22% ya taasisi za elimu nchini Burkina Faso sasa zimefungwa. Hali hii huongeza hatari ya watoto kukosa usalama, kulingana na Hubert Ouedraogo, afisa katika sirika lisilo la kiserikali la Save The Children: "Hivi majuzi tulifanya uchunguzi ambao ulionyesha kwamba wakati watoto hawawezi kwenda shul, hatari za wao kuasajiliwa katika makundi yenye silaha huwa kubwa sana. Wasichana wanapokuwa katika maeneo yenye migogoro, nafasi za wao kuolewa huongezeka kwa 20%. "

Serikali ya Burkina Faso imetoa faranga za CFA bilioni 3 ili kukabiliana na hali hii. Germaine Kaboré, Katibu wa Kiufundi wa Elimu ya Dharura. “Tunajenga maeneo ya muda ya kusomea, tunafundisha walimu kufanya shifti mbili. Pia tunafanya kozi kwa walimu wa jamii katika mitaa ambayo wazee wote wameondoka na wanafunzi wamebaki katika maeneo haya yaliyo katika hatari. "

Kwa hivyo serikali inakusudia kuwapeleka shule watoto wote wa Burkina Faso ifikapo mwisho wa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.