Pata taarifa kuu
USALAMA WA CHAKULA

Rais wa Urusi Vladimir Putin aahidi kupeleka nafaka barani Afrika

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameahidi leo Jumatatu kutuma nafaka barani Afrika ikiwa makubaliano ya mauzo ya nje ya Ukraine hayatafanywa upya katika muda wa miezi miwili, kufuatia kuongezwa kwa muda uliotangazwa Jumamosi na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Marais Xi Jinping, Cyril Ramaphosa, Vladimir Putin na Michel Temer wakipiga picha wakati wa mkutano wa kilele wa BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini, Julai 26, 2018.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Marais Xi Jinping, Cyril Ramaphosa, Vladimir Putin na Michel Temer wakipiga picha wakati wa mkutano wa kilele wa BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini, Julai 26, 2018. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa hatimaye tutaamua kutoongeza mkataba huu kwa siku 60, basi tuko tayari kutoa kutoka Urusi bila malipo kiasi chote ambacho kilikusudiwa hivi karibuni kwa nchi zenye uhitaji zaidi barani Afrika," rais wa Urusi amesema jijini Moscow mbele ya viongozi wa Kiafrika.

Kulingana na Vladimiri Puitin, Urusi "inatimiza kwa uangalifu majukumu yake yote, katika usambazaji wa chakula, mbolea, mafuta na bidhaa zingine muhimu kwa nchi za bara hilo, na hivyo kuchangia kuhakikisha usalama wa chakula na nishati". Kwa mara nyingine tena amesisitiza ukosoaji wake kwa nchi za Ulaya, akizishutumu kwa kuhodhi nafaka kutoka bandari za Ukraine.

"Ni tani milioni 3 tu za nafaka zilitumwa Afrika na milioni 1.3 kwa nchi maskini zaidi barani Afrika", amesema, dhidi ya "tani milioni 12 zilizotumwa kutoka Urusi" kwenda barani. Rais wa Urusi amesema katika hotuba yake kwamba Moscow "itaamua juu ya ushiriki wake wa baadaye" katika makubaliano ya nafaka, ambayo yaliongezwa Jumamosi hadi Mei 18, ikiwa tu "utekelezaji wa haki na kamili" makubaliano haya "utasahihishwa".

Mapema Jumatatu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi iliweka masharti ya kuendelea kwa Moscow kwa makubaliano hayo, hasa juu ya "kuunganishwa tena" kwa benki ya Rosselkhozbank kwa mfumo wa malipo wa kimataifa wa Swift, "kukomeshwa kwa vizuizi vya bima" vya meli, au "kutolewa kwa mali za kigeni na akaunti za kampuni za Urusi zinazohusiana na uzalishaji na usafirishaji wa vyakula na mbolea".

"Bila ya maendeleo katika kukidhi mahitaji haya ushiriki wetu katika (makubaliano) utasitishwa," wizara ya Urusi ilionya. Kwa hali ilivyo, "makubaliano yanaendelea kufanya kazi kwa muda wa miezi miwili ijayo ndani ya vigezo vilivyopo, bila mabadiliko yoyote katika bandari zinazohusika", wizara hiyo ilibainisha katika taarifa hii kwa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.