Pata taarifa kuu

Ajali ya treni yaua watu wawili na kujeruhi 16 nchini Misri

Ajali ya treni iliua watu wawili na kujeruhi 16 siku ya Jumanne katika mji wa Qalioub, kaskazini mwa Cairo, wizara ya afya ya Misri imesema hivi punde.

Mji mkuu wa Misri, Cairo. Mkasa mbaya zaidi wa reli katika historia ya nchi hiyo ulitokea mwaka 2002, wakati moto uliozuka katika treni ulipoua zaidi ya watu 370 yapata kilomita 40 kusini mwa Cairo.
Mji mkuu wa Misri, Cairo. Mkasa mbaya zaidi wa reli katika historia ya nchi hiyo ulitokea mwaka 2002, wakati moto uliozuka katika treni ulipoua zaidi ya watu 370 yapata kilomita 40 kusini mwa Cairo. © Andrew Shenouda / GettyImages
Matangazo ya kibiashara

Hapo awali, wizara iliripoti katika taarifa kwa vyombo vya habari "kifo chamtu mmoja na 16 kujeruhiwa", sita kati yao tayari wametibiwa.

Amezungumza muda mfupi baada ya "wawili waliofariki katika ajali ya treni ya Qalioub", akibainisha kuwa waliojeruhiwa walikuwa katika "hali shwari".

Kwa upande wake, Mamlaka ya Kitaifa ya Shirika la Reli la Misri imebaini kwamba, treni ilipoingia kwenye kituo cha Qalioub, "dereva alivuka eneo lililofungwa na treni iliendelea zaidi ya mstari unaokata dereva kuvuka na kumgonga mtu mmoja."

"Tkio hili lilisababisha kuharibika kwa injini ya trenii na behewa la kwanza," chanzo hicho kimeongeza katika taarifa.

Mwanasheria Mkuu Hamada Saoui ameamua, kwa mujibu wa taarifa rasmi, "kuunda timu ya kuchunguza ajali hiyo".

Misri, nchi yenye wakazi milioni 100, imekuwa nchi yeye ajali mbaya za treni na uharibifu ambao umeibua hasira ya wakazi kwa uzembe wa mamlaka na treni ambazo zimezeheka.

Mara kwa mara, majanga haya kwa ujumla yanachangiwa na matatizo ya miundombinu na ubovu wa treni.

Mnamo Aprili 2021, waziri wa uchukuzi alimfukuza kazi mwenyekiti wa Mamlaka ya Reli baada ya ajali mbili za treni katika muda wa chini ya mwezi mmoja na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40.

Mkasa mbaya zaidi wa reli katika historia ya nchi hiyo ulitokea mwaka 2002, wakati moto uliozuka katika treni ulipoua zaidi ya watu 370 yapata kilomita 40 kusini mwa Cairo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.