Pata taarifa kuu

Kampeni zinamalizika leo Alhamis nchini Nigeria

NAIROBI – Leo ni siku ya mwisho ya kampeni nchini Nigeria, kuelekea Jumamosi, ambapo wapiga kura zaidi ya Milioni 93 watapata fursa ya kumchagua rais mpya.

Wafuasi wa mgombea wa urais nchini Nigeria Peter Obi wa chama cha Leba wakiwa katika mkutano wa kisiasa mjini  Lagos, 11 Februari 2023.
Wafuasi wa mgombea wa urais nchini Nigeria Peter Obi wa chama cha Leba wakiwa katika mkutano wa kisiasa mjini Lagos, 11 Februari 2023. © Sunday Alamba/AP
Matangazo ya kibiashara

Kuna wagombea 18 lakini watatu ndio wanaopewa nafasi kubwa, wakiongozwa na mgombe wa chama tawala Bolu Tinubu, Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani na Peter Obi wa chama cha Leba, ambao jana walitia saini mkataba wa kudumisha amani.

Katika hatua nyingine, jeshi la polisi nchini humo linasema, limeweka mikakati ya kutosha kuhakikisha kuwa, kuna usalama siku ya kupiga kura.

Usman Baba Alkali, ni Inspekta Jenerali wa polisi nchini humo.

“Tumemhakikishia rais  kuwa tumejiandaa vilivyo kutoa usalama unaohitajika katika uchaguzi huu.” amesema Usman Baba Alkali, Inspekta Jenerali wa polisi nchini Nigeria.

Waangazili 90 wa uchaguzi mkuu wa Jumamosi nchini Nigeria, wamefanya kikao kujadili masuala muhimu yanayohusu utendakazi wao na kiongozi wa ujumbe huo rais wa awamu ya nne wa Kenya, Uhuru Kenyataa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.