Pata taarifa kuu

Taarifa za kupotosha za tawala kampeni za uchaguzi nchini Nigeria

NAIROBI – Nchini Nigeria, kuelekea uchaguzi wa urais siku ya Jumamosi, kumekuwa na ongezeko kubwa la taarifa za kupotosha, katika taifa hilo linalopitia changamoto za kiusalama, kipindi kigumu cha uchumi na uhaba wa noti mpya.

Wafuasi wa mgombea wa urais nchini Nigeria  Bolu Tinubu
Wafuasi wa mgombea wa urais nchini Nigeria Bolu Tinubu © LASG
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya kituo cha demokrasia na maendeleo, inaeleza kuwa kumekuwa na ripoti nyingi za kupotosha kuhusu kutokea kwa wizi wa kura na baadhi ya wagombea urais kuficha kiasi kikubwa cha fedha, na kusababisha uhaba wa noti mpya za Naira.

Mfano kumekuwa na taarifa ambazo zimebainika kuwa ni za kupotosha zilizosambazwa mara Elfu 14 kuwa kitita kikubwa cha fedha taslimu kilikuwa kimepatikana katika makaazi ya  mgombea wa chama tawala cha APC Bolu Tinubu.

Taarifa hizo za kupotosha zinaelezwa kusambaa kwa kasi kwa watumizi wa mitandao ya kijamii nchini humo wapatao Milioni 39, hali ambayo inatishia utendakazi wa Tume ya Uchaguzi.

Opeyemi Kehinde kutoka muungano wa watalaam wanaohakiki taarifa, anaonya kuwa iwapo upotoshaji unaoendelea hautadhibitiwa, unaweza kusababisha machafuko kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita, kwa sababu watu huamini taarifa wanazozisoma kwenye mitandao ya kijamii.

Haya yanajiri wakati huu kampeni zikielekea kufika mwisho kuelekea  siku ya upigaji kura ambapo mbali ni Tinubu, wagombea wengine wanaopewa nafasi ni mgombea mkuu wa upinzani  kutoka chama cha PDP Atiku Abukabar na Peter Obi wa chama cha Leba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.