Pata taarifa kuu
USALAMA UCHAGUZI - NIGERIA

Nigeria: Uhaba wa Noti ya Naira watishia usalama uchaguzi ukikaribia.

Nchini Nigeria, kuelekea uchaguzi wa urais Jumamosi ijayo, muungano wa wafanyakazi wa Benki wametangaza kususia kazi kwa kuhofia usalama wao.

Naira
Naira AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Hofu hii imetolewa na wafanyakazi hao baada ya waandamanaji kuharibu mashine za ATM na kuharibu majengo ya Benki jijini Lagos siku ya Ijumaa, wakilalamikia uhaba wa noti mpya za Naira.

Mchuuzi mjini  Lagos Muhammad Rabiu, amezungumza na Mwandishi wa RFI Hausa, Abdurrahman Gambo, akisema hawatatumia noti za zamani.

Hatuwezi tena kutumia noti za zamani, kununua wala kuuza, hali imeendelea kuwa mbaya. Mimi kama mfanyabishara mdogo nimetatizika sana, hatuwezi kuuza chochote hatuna fedha. Tumeathiriwa sana nashindwa hata kuchukua noti ya zamani, kwa sababu wanunuzi hawazitaki, hatuna hata tulichobaki nacho. Amesema Rabiu.  

Wiki hii rais Muhammadu Buhari anayeondoka madarakani, alitangaza kuanza kutumika kwa  noti mpya ya Naira 500 na 1, 000 lakini akaruhusu noti 200 za zamani kuendelea kutumika mpaka Aprili 10.

Tangu benki kuu kupiga maruguku noti za zamani mwezi Disemba, raia nchini Nigeria, wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa pesa taslimu.

Usalama kudodora

Wakati huu kampeni zikiendelea kote nchini, huku zaidi ya raia milioni tisini wakiatrajiwa kupiga kura katika uchaguzi wa wiki ijayo, taifa hilo linakabiliwa na kudorora kwa usalama.

Mapema siku ya Jumamosi, watu waliokuwa wamejihami walishambulia kituo kimoja cha polisi katika eneo la Ogidi, kusini mashariki mwa jimbo la Anambra.

Wapiganaji hao walianza kufyatua risasi kiholela walipokuwa wakikaribia kituoni na kurusha vilipuzi na mabomu ya petroli, wakaingia kituoni. Amesema Msemaji wa polisi Ikenga Tochukwu katika taarifa.

Machafuko katika eneo la kusini mashariki ni moja tu ya changamoto zinazovikabili vikosi vya usalama, ambavyo pia vinapambana na makundi ya kijihadi kwa zaidi ya miaka 14 kaskazini mashariki na magenge ya utekaji nyara kaskazini magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.