Pata taarifa kuu
ANGELA MERKEL - TUZO LA AMANI

Angela Merkel atunukiwa Tuzo ya Félix Houphouët Boigny

Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel ametunukiwa Tuzo la amani la Félix Houphouët Boigny linalotolewa kila mwaka na shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi elimu na utamaduni, UNESCO, katika hafla iliyofanyika nchini Ivory Coast.

Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel akitoa hotuba wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo ya Amani ya Félix Houphouët-Boigny katika Wakfu wa Félix Houphouët-Boigny huko Yamoussoukro, Februari 8, 2023.
Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel akitoa hotuba wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo ya Amani ya Félix Houphouët-Boigny katika Wakfu wa Félix Houphouët-Boigny huko Yamoussoukro, Februari 8, 2023. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Tuzo hii ya UNESCO inatunukiwa mwaka huu kwa Kansela wa zamani wa Ujerumani, Angela Merkel, katika sherehe iliyohudhuriwa na wageni kadhaa mashuhuri kutoka kanda nchini Côte d'Ivoire.

Kwa kumtunuku, Angela Merkel, Tuzo la Amani ya Félix Houphouët Boigny, jopo la majaji linaloundwa na watu 11 lilitaka kuashiria shukrani zake kwa "uamuzi wake wa kijasiri", uliochukuliwa mwaka 2015, wa kuwapokea zaidi ya wakimbizi milioni moja kutoka Syria, Afghanistan na Eritrea.

Mkutano huu ni wa kiishara zaidi katika kiwango cha kitaifa, kwani sherehe hii imewaleta pamoja viongozi watatu wakubwa katika wa siasa za Côte d'Ivoire, huku vyama mbalimbali vya kisiasa vikiwakilishwa, upinzani pamoja na chama tawala, ishara ya uwazi haswa ikiwa ni miezi michache imebakia kabla kuandaliwa uchaguzi.

Ili kuondokana na miaka ya mgogoro, raia wa Côte d'Ivoire wanapaswa kuchukua mitazamo mipya ambayo inakuza maadili ya utamaduni wa amani. Amesema Jean-Noël Loucou, Katibu Mkuu wa Wakfu wa Félix Houphouët Boigny.

Baadhi ya  viongozi wengine kutoka kanda ya Afrika waliohudhuria sherehe hii ni rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalowa, George Weah kutoka Liberia, Moussa Faki Mahamat, rais wa tume ya Umoja wa Afrika na rais Macky Sall aliwakilishwa Abdou Diouf, mfadhili wa tuzo hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa tuzo hili la Félix Houphouët-Boigny kutoka UNESCO kutunukiwa huko Yamoussoukro, mji mkuu wa kisiasa wa Côte d'Ivoire, hii ikiwa pia ni fursa ya kukumbuka sura, itikadi na sera za baba wa Taifa, aliyefariki miaka thelathini iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.