Pata taarifa kuu
KENYA- ETHIOPIA- SOMALIA- UKAME

Raia milioni 22 wanakabiliwa na njaa katika pembe ya Afrika

Zaidi ya watu milioni 22 kuanzia kusini mwa Ethiopia hadi kaskazini mwa Kenya na Somalia, wako hatarini kufa njaa kutokana na ukame mbaya unaendelea kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo.

Zaidi ya watu milioni 22 katika pembe ya Afrika wanakabiliwa na baa la njaa
Zaidi ya watu milioni 22 katika pembe ya Afrika wanakabiliwa na baa la njaa Reuters/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wataalamu, maeneo ambayo raia wake wengi ni wakulima na wafugaji, wanatarajiwa kushuhudia msimu wa tano mfululizo bila mvua, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa.

Umoja wa Mataifa unasema nchini Ethiopia watu milioni 12 wameathiriwa, huku Somalia ni watu milioni 5 na laki 6 na nchini Kenya ni watu zaidi ya milioni 4, hawa wote wanakabiliwa na njaa.

Aidha shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, idadi hii iliongezeka maradufu mwanzoni mwa mwaka uliopita kutoka milioni 13, huku watu zaidi ya milioni 1 wakilazimika kuhama makazi yao kutokana na uhaba wa maji na maeneo ya malisho.

Katika hatua nyingine, shirika la kimataifa linalohudumia watoto UNICEF, linasema karibu watoto milioni 2 kwenye nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia, wanahitaji msaada wa haraka wa matibabu ya utapiamlo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.