Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mkuu wa diplomasia ya Urusi awasili nchini Afrika Kusini

Ziara hii ya pili barani Afrika ya Sergei Lavrov katika kipindi cha miezi sita inakuja kama utangulizi wa mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai.

Bw. Lavrov amekutana na mwenzake wa Afrika Kusini, Naledi Pandor.
Bw. Lavrov amekutana na mwenzake wa Afrika Kusini, Naledi Pandor. Jacques Nelles.jpg
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov yuko nchini Afrika Kusini tangu siku ya Jumatatu asubuhi kukutana na mmoja wa washirika muhimu wa nchi yake katika bara la Afrika ambako nchi bado zimegawanyika kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na majaribio ya nchi za Magharibi kuitenga Moscow.

Mjini Pretoria, Bw. Lavrov amekutana na mwenzake wa Afrika Kusini, Naledi Pandor.

Serikali ya Rais Cyril Ramaphosa inaichukulia Afrika Kusini kuwa haina upande wowote inayoegemia katika mzozo wa Ukraine na imeelezea nia ya kuchukua jukumu la upatanishi.

"Kama Afrika Kusini, tunathibitisha mara kwa mara kwamba tutakuwa tayari kuunga mkono utatuzi wa amani wa migogoro katika bara la Afrika na duniani kote," Bi Pandor amesema katika hotuba yake, pamoja na Bw. Lavrov.

Bi Pandor amesisitiza mara kwa mara kwamba Afrika Kusini haitakubali kuingizwa katika mzozo wa Ukraine, na alizikosoa nchi za Magharibi kwa kulaani Urusi, huku akipuuza masuala mengine kama vile kukaliwa kwa mabavu maeneo ya Palestina na Israel.

Afrika Kusini imetangaza kutoegemea upande wa mzozo wa Ukraine na kujiepusha kupigia kura maazimio ya Umoja wa Mataifa, huku ikidumisha uhusiano wa karibu na Urusi, mshirika wa muda mrefu wa African National Congress (ANC, chama tawala) wakati kilipokuwa vuguvugu la ukombozi linalopinga utawala wa wazungu wachache wakati wa ubaguzi wa rangi.

Jeshi la Afrika Kusini linatazamiwa kufanya mazoezi ya pamoja na Urusi na China kwenye pwani yake ya mashariki kuanzia Februari 17 hadi 27, ambayo inahatarisha kuongezeka kwa mvutano kati ya Marekani na nchi za Ulaya.

Zoezi hilo litafanyika sambamba na maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Urusi Februari 24 nchini Ukraine.

Kulingana na shirika la habari la Urusi TASS, meli ya kivita ya Urusi iliyo na silaha za kivita za kizazi kijacho itashiriki katika mazoezi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.