Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Wanajeshi saba wauawa katika shambulio jipya katika kambi ya kijeshi Somalia

Wanajeshi saba wameuawa nchini Somalia katika shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi, shambulio linalodaiwa na wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali wa Al-Shabab, katika mji uliochukuliwa hivi karibuni na vikosi vinavyounga mkono serikali, wizara ya habari imetangaza leo Ijumaa.

Askari wa jeshi la Somalia akilinda eneo tukio baada ya shambulio la Al Shabab mjini Mogadishu mnamo Agosti 2022.
Askari wa jeshi la Somalia akilinda eneo tukio baada ya shambulio la Al Shabab mjini Mogadishu mnamo Agosti 2022. AFP - HASSAN ALI ELMI
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa Al Shabab "wamefanya shambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi huko Galcad", mji ulioko takriban kilomita 375 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, serikali imetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari, ikibaini kwamba kumetokea 'mapigano makali'.

Kulingana na mamlaka, askari saba, ikiwa ni pamoja na kamanda wa kijeshi, wameuawa, pamoja na wanamgambo zaidi ya mia moja wa Al Shabab. Shambulio hilo limedaiwa na kundi la Al Shabab, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda.

Al Shabab "imelipua lori mbili zilizokuwa na vilipuzi kabla ya kuanza kwa mapigano ya ana kwa ana, walifanikiwa kwa muda mfupi kuwaondoa wanajeshi nje ya kambi, lakini vikosi vya usalamaliwasili na wapiganaji wa Al Shabab wakaondoka," mkazi wa Galcad Abdilahi Rage ameliambia shirika la habari la AFP. kwa simu.

Gutale Mohamed, mkazi mwingine wa mji huo, amesema mapigano yalidumu "takriban saa moja".

Waislam wenye itikadi kali walifanya mashambulizi mengine kwenye kambi ya kijeshi siku ya Jumanne huko Hawadley, mji ulioko kilomita 60 kaskazini mwa Mogadishu. Odowaa Yusuf Rage, mkuu wa jeshi, aliiambia redio ya serikali kwamba wanajeshi watano, akiwemo afisa mmoja, "walikufa shahidi katika mapigano hayo".

Siku moja kabla, jeshi la Somalia lilitangaza kuwa limechukua, bila mapigano yoyote, Harardhere, mji wa bandari ulioko karibu kilomita 500 kaskazini mwa Mogadishu uliokuwa umedhibitiwa tangu 2010 na Al Shabab. Serikali ilihakikisha kwamba kurejeshwa kwenye himaya yake kwa jiji hili 'la kimkakati' ni 'ushindi wa kihistoria'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.