Pata taarifa kuu
USALAMA-UGAIDI

Wanajeshi 11 wauawa katika shambulizi la Al Shabab kwenye kambi ya kijeshi Somalia

Wanajeshi 11 wmeuawa katika shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi, shambulio ambalo linadaiwa na wapiganaji wa Kiislamu wenye itikadi kali wa Al Shabab, kamanda wa wanamgambo wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP leo Jumanne, siku moja baada ya serikali kutangaza kuuteka tena mji wa kimkakati.

Kikosi cha wanajeshi wa Somalia wakipiga doria katika moja ya mitaa ya Mogadishu.
Kikosi cha wanajeshi wa Somalia wakipiga doria katika moja ya mitaa ya Mogadishu. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

"Wanajihadi wamelipua kwanza gari lililokuwa na vilipuzi, kisha kushambulia kambi ya kijeshi huko Hawadley", yapata kilomita 60 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, amesema Mohamed Osman, kamanda wa wanamgambo wa eneo hilo wanaoshirikiana na utawala, aliyehojiwa kwa simu na shirika la habari la AFP. Wanajeshi 11, akiwemo kamanda mmoja, wameuawa na "magaidi kadhaa pia wameuawa", ameongeza. Shambulio hilo limedaiwa na kundi la Al Shabab, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda.

"Shambulio lilianza kwa mlipuko mkubwa kabla ya makabiliano ya moja kwa moja (na jeshi) huko Hawadley. Wanamgambo wa Al-Shabab walivamia kambi ya kijeshi kwa muda mfupi na kuchoma moto baadhi ya mali, kumeripotiwa na majeruhi", Idris Hassan, mkazi wa mji jirani, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Taarifa za awali tulizozipata zinaeleza kuwa zaidi ya watu kumi wameuawa katika shambulio hilo, lakini bado hatujathibitisha taarifa za watu waliopoteza maisha. Lakini naweza kuthibitisha kwamba magaidi hao wametimuliwa na kwamba jeshi la Somalia lina udhibiti kamili wa eneo hilo," kamanda wa jeshi la Somalia Ahmed Mohamud, ambaye yuko katika mji wa Balcad, mji ulio karibu na Hawadley, ameliambia shirika la habari la AFP.

Al Shabab wamekuwa wakipigana na serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa tangu 2007. Wapiganaji hao ambao walitimuliwa nje ya miji mikuu ya nchi mwaka 2011-2012, wamesalia imara katika maeneo makubwa ya vijijini.

Rais Hassan Cheikh Mohamoud, ambaye alirejea madarakani mwezi Mei 2022, ameahidi "vita kamili" dhidi ya kundi la Kiislamu, na hivi majuzi aliwaita wapiganaji wa kundi hili "kunguni".

Siku ya Jumatatu, jeshi la Somalia lilitwaa Harardhere, mji wa bandari uliochukuliwa kuwa "wa kimkakati" na mamlaka ilioko takriban kilomita 500 kaskazini mwa mji mkuu, unaodhibitiwa na Al Shabab tangu 2010.

Serikali ya Hassan Sheikh Mohamud imeahidi "vita vya kila namna" dhidi ya kundi hili la Kiislamu, ambapoo wapiganaji wakeBw Mohamoud hivi majuzi aliwaita "kunguni". Mnamo mwezi Septemba, alituma jeshi, ikiwa ni pamoja na vikosi maalum, kusaidia wanamgambo wa ndani, wanaojulikana kama "Macawisley", ambao waliasi dhidi ya Al Shabab.

Mashambulizi haya, yakiungwa mkono na jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis) na mashambulizi ya anga ya Marekani, yalifanya iwezekane kuteka tena maeneo makubwa katika majimbo mawili katikati mwa nchi, Hirshabelle ambako kunapatikana mkoa wa Hiran na Galmudug.

Lakini Al Shabab wanaendelea kufanya mashambulizi ya umwagaji damu kulipiza kisasi. Watu 19 waliuawa katika mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari huko Mahas, mji wa Hiran, mapema mwezi huu.

Tarehe 29 Oktoba, magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu yalilipuka ndani ya dakika chache katika mji mkuu Mogadishu, na kuua watu 121 na wengine 333 kujeruhiwa, katika shambulio baya zaidi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika katika kipindi cha miaka mitano.

Rais ametangaza kwamba vikosi vipya vya wanajeshi wa Somalia, waliofunzwa nchini Eritrea, hivi karibuni vitatumwa katika operesheni dhidi ya Al shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.