Pata taarifa kuu
NIGERIA - USALAMA-UCHAGUZI

Nigeria: Uchaguzi utaendelea kama ulivyopangwa

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, Mahmood Yakubu amesema licha ya changamoto za kiusalama hasa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 25 mwezi Februari, utaendelea kama ilivyopangwa.

Mahmood Yakubu, Rais wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria.
Mahmood Yakubu, Rais wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria. KOLA SULAIMON/AFP/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

“Licha ya mashambulio ambayo tumeshuhudia na kupata hasara, tutajenga upya miundombinu yote iliyoharibiwa.”amesisitiza Mahmood Yakubu.

Ametoa hakikisho hili, baada ya hapo awali kudokeza kuwa kuna wasiwasi wa uchaguzi huo kufanyika kwa sababu ya utovu wa usalama.

Watu Milioni 93.4 wameandikishwa kama wapiga kura katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.